Yanga SC wapo kwenye mazungumzo na Aziz KI juu ya mkataba mpya

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Ally Kamwe ameweka wazi kuwa Staa wao Aziz KI ana maliza Mkataba wake Yanga SC mwisho wa msimu ila wapo kwenye mazungumzo nae.

“Mimi siwezi kuwekeza nguvu kwenye siasa na sitaki kudanganya Wanachama wa Yanga, nawaambia uhalisia mapema wajue nini tunatakiwa tufanye”

“Aziz Ki ni Mchezaji wa Yanga ana Mkataba hadi mwisho wa msimu, mpaka sasa hivi tuko kwenye mazungumzo nae lakini Aziz KI hajasaini Mkataba mpya huo ndio ukweli sitaki kuwekeza kwenye siasa”

Hadi sasa Aziz KI amekuwa akihusishwa kuwindwa na Vilabu vya Mamelod Sundowns na Kaizer Chiefs vya Afrika Kusini pamoja na Club moja wapo ya Qatar.

Related Posts