Mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) kati ya Yanga dhidi ya Azam FC sasa utapigwa Juni 2, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar badala ya ule wa Tanzanite ulioko Babati, Manyara.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa taarifa hiyo ambayo uamuzi wa kubadilisha uwanja umefanywa na kamati ya utendaji ya shirikisho hilo baada ya kubaini baadhi ya miundombinu ya mjini Babati haiku tayari kwa fainali hizo pamoja na sababu za kiusalama.
Aidha shirikisho imezishauri mamlaka za soka mkoani Manyara kuendelea kufanyia maboresho miundombinu ya viwanja vyao ili kufikiriwa zaidi kwenye fainali au mashindano mengine.
Shirikisho limeongeza, limemualika Waziri wa Habari, vijana na Utamaduni Zanzibar, Tabia Maulid Mwita kuwa mgeni rasmi kwenye fainali hizo.