MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewasisitiza wafanyabiashara wote nchini hasa wa jiji la Dar es Salaam kulipa Kodi bila kushurutishwa kwani kwani ni kipindi cha mwisho wa mwaka wa fedha 2023/2024.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 22, 2024 amesema kuwa Amesema kuwa lengo la mazungumzo hayo ni kuwakumbusha, kuwa sisitiza wafanyabiashara na watu wote wanaotakiwa kulipa kodi na kulipa kwa wakati.
Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ameamua kujenga nchi kwa kutumia falsafa ya kujenga upya nchi yetu, mabadiliko ya sheria ndogondogo na kubwa, ustahimilivu pamoja na maridhiano hivyo wafanyabiashara wenye changamoto wanatakiwa kufuata misingi hiyo.
Kwa upande wa wanaouza vinywaji baridi na moto Chalamila amewataka kuhakikisha vinywaji hivyo vimethibitishwa na vinastika kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa sababu kushindwa kufanya hivyo ni kuihujumu Afya ya mtumiaji na kuhujumu mapato ya nchi.
Aidha, Migomo ya baadhi ya wafanyabiashara pale TRA wanapohitaji kutumiza majukumu yao. Chalamila ametoa rai kwa wafanyabiashara kutoa ushirikiano kwa TRA kwani taasisi hiyo inatambulika kisheria.
Pia amewakumbusha wafanyabiashara kuwa Tanzania si nchi ya vita bali ni nchi ya maridhiano…. “Huu ni muda wa kukimbia mchakamchaka na kufanya biashara bila shida kwani Serikali ya Rais Samia ipo tayari kusikiliza na kufanya mabadiliko pale panapohitajika. ” Amesema Chalamila
Licha ya hayo Chalamila amesema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa TRA kuhusu wafanyabiashara kutoa risiti za bidhaa zinazokinzana na malipo halali yaliyofanyika.
“Nawakumbusha wafanyabiashara biashara wote kutoa risiti halali kwani kushindwa kutoa risiti halali za Kieletroniki (EFD) ni kulihujumu taifa, pia ikumbukwe kuwa mfanyabiashara ni wakala wa kukusanya Pesa kutoka kwa mwananchi kwenda Serikalini kupitia TRA. ” Amesema
Sambamba na hayo Chalamila aliwataka wafanyabiashara kutoka maeneo jilani kuja kufanya biashara Mkoa hapa.
“Kipindi cha nyuma wafanyabiashara wengi walilalamika na kukimbia nchini kwetu kutokana na kuumizwa na namna ya ukusanywaji kodi ulivyokuwa ukifanyika, lakini katika uongozi wa Rais Samia wafanyabiashara wengi wamerudi nchini na wanafanya biashara bila shida hivyo ungeni mkono juhudi zake kwa kutambua majukumu yenu na kwa kushirikiana na kamishna wa TRA, Alphayo Kidata.” Amesema.