Tanzania, Msumbiji wajadili mikakati kuinua biashara, uwekezaji

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine Kasike amekutana na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Msumbiji, Silvino Augusto José Moreno na kukubaliana kufanikisha ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).


Pia katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jana Jumatano kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Jijini Maputo, viongozi hao wamekubaliana kutafuta mbinu na mikakati mahsusi ya kuongeza  kiwango cha biashara baina nchi hizi ili kiende sambamba na uhusiano wa kindugu, kihistoria na kijiografia baina ya nchi hizi.

Moja ya maeneo yaliyopendekezwa ni kuanzisha  Jukwaa la Pamoja la Biashara litakalowakutanisha wafanyabiashara na wadau wengine muhimu ili kubadilishana uzoefu, kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi na kubaini namna ya kunufaika nazo.

Related Posts