Maaisita kutoka Shule ya Mtakatifu Maria Goreti ya Mjini Moshi wamesema kwa sasa Jeshi la Polisi limekuwalikionekana kuanza kubadilika katika utendaji kazi wao huku wakibainisha kuwa endapo mabadiliko hayo yakoendelea imani kwa wananchi itakuwa kubwa zaidi kwa Jeshi la Polisi.
Hayo wameyabainisha walipofika katika shule ya Polisi Tanzania kuhudhuria halflang ya kuvishwa Nishani ambapo walipata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa mawasiliano katika Shule ya Polisi Tanzania.
Masisita hao kutoka shule hiyo walipata maelezo mafupi ya Shule ya Polisi Tanzania baada ya hafla ya kuvishwa Nishani kwa Maafisa na wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali iliyofanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Angela Kibiriti ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shule ya PolisiTanzania katika picha akiwapa maelezo mafupi masisita hao.
Masisita hao ambao ni Samwela Dominiki, Clementina Kachweka na Edwina Mushi ambao wote wanatoka Shule ya Mtakatifu Maria Goreti (St. Maria Goreti) wamefurahishwa kwa namna ambavyo Jeshi la Polisi kwasasa limejikita katika kutoa huduma bora na maboresho ya kitaaluma ambapo wamesema kuwa endapo wataendelea kubadilika wategemee imani kuendelea kukua kwa wananchi Juu ya Jeshi hilo.