Na Yeremias Ngerangera …Songea.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Meneja wa Tanesco Mkoa wa Ruvuma Eliseus Mhelela alisema vijiji vinavyopata umeme vimeongezeka kutoka vijiji 489 mwezi marchi 2024 Hadi kufikia vijiji 538 mwezi mei 2024.
Mhelele alisema ongezeko Hilo linatokana na kazi zinazofanywa na wakandarasi walioko katika vijiji mbalimbali wakiendelea na kazi ya kusambaza huduma ya umeme katika vijiji ambavyo Bado havijapata huduma hiyo.
Aidha Mhelela alidai mpaka kufikia mwezi marchi 2024 vijiji vilivyopata umeme vilikuwa 489 sawa na asilimia.88.3 ya vijiji vyote 554 vya Mkoa wa Ruvuma na vikabakia vijiji 65.
Mpaka mwezi mei 2024 Mhelela alisema vijiji vilivyopata umeme vimeongezeka kutoka 489 mwezi marchi 2024 mpaka kufikia vijiji 538 mwezi mei 2024 sawa na asilimia 97.1
Mhandisi wa Tanesco Mkoa wa Ruvuma Malibe Jastine Boniphace alidai vijiji vilivyobaki kupatiwa huduma ya umeme ni vijiji 16 ambavyo wakandarasi wapo wanaendelea na kazi ya kusambaza huduma ya umeme katika vijiji hivyo vilivyobaki.
Hata hivyo Boniphace aliwataja wateja ambao wananufaika kupitia mradi wa REA 3 mzunguko wa pili katika Mkoa wa Ruvuma ni wateja 5214.
Mkoa wa Ruvuma una jumla ya vijiji 554 na kati ya vijiji hivyo Tanesco imefanikiwa kufikisha huduma ya umeme katika vijiji 538 na kubakiwa na vijiji 16 Pekee mpaka Sasa.