RC MAKONDA ATATUA TATIZO LA UMEME ZAHANATI YA LEREMETA – LONGIDO

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul
Makonda ametembelea na kukagua utoaji huduma katika zahanati ya kijiji
cha Leremeta ambapo amehoji kuhusu umeme unaopatikana katika zahanati
ili kujua unawezesha mitambo yote kufanya kazi ipasavyo.


Katika
majibu yake, uongozi wa zahanati hiyo umesema kuwa umeme hauridhishi
kwakuwa ni single phase na moto unaopatikana ni mdogo hali inayopelekea
hata kipimo kidogo cha damu kutoweza kufanya kazi.

Naye, Meneja
TANESCO Longido Mhandisi. Lazaro Lenoi, mara baada ya kuulizwa na RC
Makonda kuhusu uwepo wa umeme mdogo katika zahanati hiyo, amesema
waliunganisha umeme wa single phase kwakuwa ndivyo mahitaji yao
walivyoomba kutoka uongozi wa zahanati hiyo.

Kutokana na maji
hayo, RC Makonda alimuhoji tena Mhandisi. Lazoro kuwa kwanini baada ya
kupata malalamiko kwanini asingefika katika zahanati hiyo kushughulikia,
jambo ambalo Meneja TANESCO amesema hajapokea malalamiko wala
changamoto yoyote tangu walipounganisha umeme huo.

RC Makonda
aliongeza swali kwa Meneja TANESCO na kumuuliza kwanini hakutumia
utaalamu wake kutoa ushauri kwa uongozi wa zahanati hiyo ili kuwavutia
umeme wa three phase, jambo ambalo amesema alishamueleza Mwenyekiti wa
serikali ya kijiji ilipo zahanati hiyo.

Naye, Mwenyekiti wa
serikali ya Kijiji Mhe. Supuk Melita, mara baada ya kuulizwa na RC
Makonda kuhusu ushauri huo, amekiri kuwa walipokea ushauri huo.

Mara
baada ya kusikiliza pande zote mbili, RC Makonda ameamua kutoa kiasi
cha fedha zaidi ya Tsh 100,000/= kuunganishwa kwa three phase katika
zahanati hiyo ndani ya siku tatu.

“… hapa ni zahanati na
imetumika fedha kwaajili ya kuhakikisha wananchi wa kijiji hiki
wanapatiwa huduma ya afya stahiki.. lazima tuwe sehemu ya kumsadia kazi
vizuri Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , kwa kutafsiri kazi
yake kwa wananchi wa hali ya chini “

” Umeme uunganishwe hapa wa kutosha kwenye zahanati na kwenye nyumba ya watumishi “

 

Related Posts