WAZIRI MCHENGERWA ATOA MWEZI MMOJA UKAMILISHAJI WA KITUO CHA AFYA RUAHA.

ULANGA

Waziri wa Nchi, @ortamisemitz Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Ruaha baada ya ujenzi wa kituo hicho kutokamilika kwa wakati.

Mhe. Mchengerwa ametoa agiza hilo Mei 22, 2024 baada ya kuanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo na kutembelea Kituo cha Afya cha Ruaha na kubaini ujenzi wa kituo hicho umechukua muda mrefu kitu kimachoonesha kutokuwajibika kwa viongozi wa Halmashauri hiyo.

Amesema, mradi huo uliibuliwa na wananchi tangu mwaka 2019 hadi sasa haujakamilika pamoja na jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima kuhakikisha mradi huo unakamilika lakini kumekuwa na vikwazo vinavyosababisha wananchi kukosa huduma ya Afya.

Waziri Mchengerwa hakuridhishwa na kasi ya ujenzi huo na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uanga pamoja na timu yake kukamilisha ujenzi huo ifikapo Juni 30 mwaka huu bila kuwa na nyongeza ya muda mwingine

“ninawataka Kila mmoja wenu kufanya kazi usiku na mchana Kituo hiki kikamilike tarehe 30 mwezi wa sita hakuna nyongeza’

Sambamba na maagizo hayo ametumia fursa hiyo kumpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Salim Hashim kwa kutoa fedha shilingi milioni kumi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Afya cha Ruaha ili kuhakikisha wapiga kura wake wanaondokana na usumbufu wa kufuata huduma ya Afya umbali mrefu.


Related Posts