*OR-TAMISEMI ,TRA zapewa ushauri na CAG
Na Chalila Kibuda,Michuzi Blog
Halmshauri ya Singida mkoani Singida yatumia malipo ya sh. Milioni 147.29 yaliyodhibitishwa na Stakabadhi Bandia ‘Fake’
Kwa Mujibu wa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) CPA Charles Kichere pya Mwaka wa Fedha 2023/2023 ilisema kuwa katika ukaguzi alibaini kwa malipo yenye thamani ya Sh. milioni 147.29 yaliyothibitishwa na stakabadhi bandia za kielekitroni katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida.
Katika Ripoti hiyo hiyo CAG amependekeza OR-TAMISEMI ishirikiane na Wizara ya Fedha na
Mamlaka ya Mapato (TRA) kuhuisha mfumo wa ulipaji serikalini (MUSE) na mfumo wa kodi, ambapo taasisi za umma zitaweza kujiridhisha na taarifa za kikodi za wazabuni na watoahuduma mbalimbali
waliosajiliwa na TRA pamoja na kuthibitisha usahihi wa makato ya kodi kabla ya kuidhinisha malipo yao.
Pia CAG ameshauri katika ripoti hiyo TRA kuongeza ufuatiliaji wa kubaini wafanyabiashara
wasio waaminifu ambao hawatoi stakabadhi za kielekitroni na kuwachukulia hatua stahiki kwa mujibu.
Ripoti hiyo Halmashauri hiyo imetumia fedha hiyo malipo hewa ambayo ya kufanyika kwa vielelezo bandia