Dc Nsemwa ahamasisha michezo kwa watumishi

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mhe. Rebecca Nsemwa ametoa Wito kwa wafanyakazi kuwa na utamaduni wa Kufanya mazoezi mara kwahe mara Ili kuepukana na magonjwa yasiyo ambukiza.

Dc Nsemwa amesema hayo wakati aliposhiriki bonanza la Michezo lililoandaliwaJeshi na (JWTZ) Shirika la Mzinga la Kikosi cha Mazao yaliyofanyika Katika viwanja vya shirika hilo

Dc Nsemwa amesema Shirika la Mzinga na Mazao Kwa kuendendea kuandaa mabonza ya michezo mara kwa mara kwa wafanyakazi hao ili kuwaweka pamoja na kuwakutanisha na Jamii.

Amesema Ili mtumishi afanye kazi kwa weredi anatakiwa awe na afya njema hivyo mazoezi ya mara kwa mara yanasaidia kuimarisha afya.

Kwa upande wake Meneja Shirika la Mzinga na Mazao Brigedia Jenarali Seif Hamisi amesema lengo la Michezo hiyo kuimarisha afya Kwa wafanyakazi pamoja kuwaweka pamoja ambapo michezo hiyo itakayo chezwa ni pamoja na Mpira wa miguu,kuvuta tamba,riadha, Mpira wa kikapu na Mpira wapete.

Amesema mwaka huu Michezo hiyo imeboreshwa na kwamba wananchi na vikundi mbalimbali vinashiriki Ili kuonesha vipaji mbalimbali.

Related Posts