Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Pwani Jennifer Shirima akitoa mada kwa waandishi wa habari na wadau wa habari kuhusu umuhimu wa kuwahi kutoa taarifa za majanga ya moto na ajali pindi zinapotokea.
Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Pwani wakiwa katika picha ya Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge
“Kuna usemi usemao kizuri chajiuza hivyo nao hawana budi kujiuza ndani ya Mkoa wa Pwani kuna kiwanda kinatengeneza Flat Screen TV nai anajua hakuna, sasa kama unazalisha bidhaa nzuri halafu hujitangazi soko lako litapatikana wapi”.
“Mbali ya kusisitiza umuhimu wa wawekezaji kutumia vyombo vya habari pia Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani amewasisitiza waandishi wa habari kuandika habari kwa kutumia mbinu ambazo zitawavutia zaidi wenye viwanda na kuwapa ushawishi na faida watakazozipata pindi watakapo tumia vyombo hivyo vya habari.
Nasisitiza kwa kutoa shukrani zangu kwa vyombo vya habari vya Mkoa wa Pwani sababu binafsi nathamini mchango wa wanahabari kwakuwa wanafanya kazi kubwa katika kuleta maendeleo ndani ya Mkoa.
RC Kunenge amesema hayo Mei 23 wakati akifunga maadhimisho ya siku ya Vyombo vya habari kimkoa katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wq Pwani uliohudhuriwa na wadau wa habari mbalimbali waandishi wa habari na Maafisa Habari wa Mkoa wa Pwani.
Mkutano huu umeandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Mkoa wa Pwani (CRPC).
“Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani kazi zenu mnazozifanya zinaonekana hivyo nasema wazi kwamba nathamini mchango wenu”amesema Kunenge.
Aidha katika hatua ingine Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa anaguswa na hali ya uchumi duni ya waandishi huku akisisitiza kwamba haimfurahishi huku akisisitiza kuwa ataweka mazingira wezeshi ambayo yatasaidia waandishi kua nanuchumi madhubuti kwa sababu wako ndani ya Mkoa wenye viwanda na tajiri nchi nzima.