Maafisa hao ni wa ngazi za juu zaidi nchini Syria kushitakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinaadamu katika mahakama ya Ulaya.
Mashitaka dhidi yao yalihusisha kisa cha kupotea kwa raia wenye uraia pacha wa Syria na Ufaransa ambao ni Mazzen Dabbagh pamoja na mwanae Patrick waliokamatwa na maafisa hao, na baadae waliripotiwa kufariki wakiwa korokoroni.
Kesi ya maafisa hao watatu iliendeshwa kwa siku nne wakiwa hawapo mahakamani. Miongoni mwao ni Ali Mamlouk, aliyekuwa mkuu wa Ofisi ya Usalama wa Taifa ambaye bado anahudumu kama mshauri wa usalama katika ofisi ya Rais wa Syria Bashar al-Assad.
Soma pia: Kiongozi wa zamani wa wanamgambo Syria ashitakiwa Ujerumani
Wengine ni Jamil Hassan, aliyekuwa mkurugenzi wa idara ya ujasusi kwenye jeshi la anga na Abdel Salam Mahmoud, aliyekuwa mkuu wa upelelezi.