Maafisa forodha mpaka wa Tunduma,maafisa ardhi Mbeya na Songwe wapatiwa elimu juu ya matumizi ya Zebaki

Maafisa Forodha wa mpaka wa Tunduma na Maafisa Mazingira wa Mikoa ya Mbeya na Songwe wapatiwa mafunzo juu ya Muungozo wa Uingizaji na Utumiaji wa kemikali ya Zebaki nchini.

 

Mafunzo hayo yametolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika ofisi za mpaka wa Tunduma Mkoa wa Songwe.

Akitoa mafunzo hayo, Boniface Kyaruzi Mhandisi Mazingira wa NEMC amesema ni kwa lengo la kuwajengea uelewa wa namna sahihi ya usimamizi, uingizaji halali na matumizi salama ya kemikali ya zebaki kwa wachimbaji wadogo ili kuepuka athari za kiafya na kimazingira

 

Bwana Kyaruzi ameongeza kuwa mafunzo haya yanayoendeshwa kupitia Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Kemikali ya Zebaki (EHPMP) unaofadhiliwa na Benki Kuu ya Dunia na kuratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ni mahususi kwa ajili ya utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa MINAMATA wenye takwa la kuandaa mpango kazi wa Kitaifa kwa kil Nchi mwanachma wa namna sahihi ya kudhibiti matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo kwa dhumuni la kulinda afya ya binadamu na mazingira dhidi ya madhara yanayotokana na uchafuzi unaotokana na zebaki.

Naye Bw. Jansen Bilaro Mkemia kutoka Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mbeya alipozungumza amewataka Maafisa hao kushirikiana bega kwa bega na Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kudhibiti uingizaji haramu na matumizi yasiyo salama ya kemikali ya zebaki kwa kuhakikisha waingizaji, wasambazaji na wachimbaji wadogo wanasjiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kemikali Na.3 ya mwaka 2003 inayohusu usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani ikiwemo zebaki. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Ofisi ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na Ofisi ya Tume ya Madini Mkoa wa Mbeya watoa mafunzo ya matumizi salama ya kemikali ya zebaki kwa Wachimbaji wadogo wa madini wa Kata ya Saza, Kijiji cha Patamela Wilaya ya Songwe Mkoa wa Mbeya.

Akizungumzia mafunzo hayo, Mhandisi wa Mazingira NEMC, Boniface Kyaruzi amesema mafunzo hayo yanaendeshwa kupitia Mradi wa Kudhibiti Mtumizi ya kemikali ya Zebaki unaofadhiliwa na Bank ya Dunia na baraza hilo ambapo Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepewa jukumu la kutoa elimu kufuatia takwa la mkataba wa Minamata.

 

“Sambamba na hilo kufuatia Kaulimbiu ya Siku ya Mazingira Duniani isemayo, Urejeshwaji wa Ardhi iliyoharibiwa na Ustahimilivu wa Hali ya Jangwa na Ukame, tumewakumbusha wachimbaji wadogo kuhakikisha wanarejesha mazingira ya ardhi iliyoharibiwa kutikana na uchimbaji wa madini katika hali yake mara baada ya kumaliza shughuli za uchimbaji ili kuhakikisha ardhi inakua endelevu kwa matumizi mengine,”.

Related Posts