Wadau watoa pikipiki 10 kuimarisha usalama mkoani Arusha

Wadau wa masuala ya usalama wamekabidhi Pikipiki 10 kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda kwa ajili ya kulisaidia Jeshi la Polisi katika kuimarisha usalama Mkoani humo ambao ni muhimu na kitovu cha Utalii hapa Nchini.


Akipokea pikipiki hizo zilizotolewa na Kampuni ya Multicable Limited (MCL), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda amesema pikipiki hizo zinakamilisha ahadi yake ya kulipatia Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha pikipiki 50 huku akibainisha hatua inayofuata nikukamilisha ahadi ya kutoa pikipiki za umeme 100 pamoja na magari 20.

Mheshimiwa Makonda amesema lengo lake ni kuhakikisha Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa ufanisi kwa kuwa na vifaa vya kisasa na vya kutosha vitakavyosaidia kubaini na kuzuia uhalifu kabla ya kutokea kuhakikisha mkoa huo unaendelea kuwa shwari hasa kwa kuzingatia ni kitovua cha utalii hapa nchini.

Akikabidhi Pikipiki hizo Bwana Hussein Ali Bhai na Bwana Murtaza Ali Bhai ambao ni Wakurugenzi wa Kampuni hiyo yenye makao makuu yake Jijini Dar Es Salaam wamesema wamekuja kuunga juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kampeni yake ya kuufanya Mkoa huo kuwa sehemu salama.

Aidha wamebainisha kuwa waliona utendaji kazi wake wa kuonesha nia ya kulisaidia Jeshi la Polisi vitendea kazi kwa ajili kufanya shughuli zake za ulinzi wa raia na mali zao, hivyo wakaona ni vyema kuunga mkono juhudi hizo ili kufikia lengo la kuufanya mkoa huo kuwa salama wakati wote.

 

Related Posts