Na Chalila Kibuda ,Michuzi
Manispaa ya Temeke ya katika ripoti ya CAG iliweza kutumia kiasi cha sh.155,839,175 Kwa vifaa ambavyo havijavidhibishwa ubora.
Hayo yamebainika katika Ripoti ya CAG ambapo ni mlolongo wa Halmashauri nyingi kufanya hivyo ikiwemo Manispaa ya Temeke
Ripoti hiyo imesema kufanya matumizi ya vifaa bila kuangaliwa ubora Kwa kudhibitishwa na mamlaka zilizoidhinishwa.
Kufanya malipo na mapokezi ya bidhaa na huduma bila kukaguliwa na kamati husika kunaweza kuhatarisha ubora na ulinganifu wa vipimo,na inaweza kusababisha upatikanaji wa bidhaa duni au zisizo na ubora.
Ninapendekeza mamlaka za serikali za mitaa zizingatiekanuni za Ununuzi kwa kukagua ubora na wingi wa bidhaa na huduma zilizonunuliwa kabla ya kupokea na kufanya malipo kwa wazabuni.
Ripoti hiyo ilisema Matumizi ya vifaa vya ujenzi bila kufanyiwa vipimo vya ubora -Sh. bilioni 1.52 katika baadhi ya Serikali za Mitaa wa Halmashauri na Manispaa.
Kanuni ya 244(1) ya Kanuni za Ununuzi wa umma (2013) inasema, bidhaa zitakazowasilishwa zinahitajika kukaguliwa, zichukuliwe sampuli na kupimwa na taasisi inayofanya ununuzi; na hazitokubalika kama zitakuwa chini ya viwango vilivyobainishwa kwenye mkataba.
Pia, Kanuni ya 246 inasema kuwa, ikiwa bidhaa itahitaji jaribio la kiufundi au la kisayansi, mtaalamu au mjuzi wa taaluma husika ataalikwa kwa mashauriano, au bidhaa zaweza kutumwa kwa mjuzi huyo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Ripoti ilibaini mamlaka 16 za serikali za mitaa zilinunua na kutumia vifaa vya ujenzi, zikiwamo nondo na matofali, vyenye thamani ya Sh. bilioni 1.52 katika miradi ya ujenzi bila kufanyiwa vipimo vya ubora.
Hata hivyo Manispaa hiyo ilifanya manunuzi nje ya mfumo wa sh.2669,567,475 ambapo ni tofauti na miongozo iliyowekwa.