DC Tanga awaomba wamiliki wa vyuo vikuu kuanzisha matawi ya vyuo vyao Tanga.

Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe Jeams Kaji amewataka wamiliki wa vyuo vikuu hapa nchini kuangalia uwezekano wa kuanzisha matawi ya vyuo vyao mkoani tanga ili kukuza uchumi wa mkoa wa tanga.

Dc Kaji ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika maadhimisho ya kitaifa ya wiki ya elimu, ujuzi na ubunifu yanayo fanyika kitaifa Mkoani Tanga yenye kaulimbiu ya Elimu,Ujuzi na ubunifu kwa uchumi shindani na kuwataka wamiliki wa vyuo vikuu hapa nchini kuweka mkakati wa kuanzisha vyuo hivyo mkoani tanga ili kuwezesha ukuaji wa uchumi.

“hii ni bahari kubwa sana kwetu kama wananchi wa mkoa wa Tanga kwani ukizingati Tanga hatuna chuo kikuu hata kimoja hivyo nivyema wananchi kuweza kuja na kuwaleta watoto wao kuja kujiunga na vyuo mbalimbali Pamoja na kujifunza fursa zitokanazo na uwepo wa maadhimisho hayo.

“wananchi wa tanga wamekuwa na vilio vyingi sana hususa ni kwenye mitandao ya kijamii juu ya kulalamikia ukosefu wa chuo kikuu mkoani hapa hivyo niwaombe wadau wa vyuo vikuu wenye nia ya kuanzisha matawi ya vyuo hivyo waje ili tuweze kuwapa maeneo kwaajili ya kuanzisha vyuo hivyo.’’

Aiadha mkuu wa wilaya ameongeza kuwa endapo yataanzishwa matawi ya vyuo hivyo itatoa fursa ya wafanyakazi kuweza kusoma masomo ya jioni ili kuweza kujiendeleza kielimu kwa ngazi ya juu.

Kwaupande wake meneja mkuu wa tasisi ya Global Education link Regina Lema amewataka wanafunzi wa kada mbalimbali wanaopenda kusoma nje ya nchi kujitokeza ili kuweza kupata nafasi za kusoma nje ya nchini kwani kunazaidi ya vyuo 400 kutoka ndani nan je ya nchi.

Katika hatua nyengine Regina amesema kuwa wanafunzi wanao soma nje ya nchi wanapata fursa nyingi kwa kuweza kusoma huku wanafanya kazi, lakini pia wanaweza kupata mikopo usio kuwa na riba kwa wanafunzi wanao hitaji kusoma nje ya nchini.

Related Posts