NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
KLABU ya Yanga imeendelea kutamba mbele ya watani wao Simba Sc mara baada ya kufanikiwa kuichapa 2-1 kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo ambao Yanga walianza kupata bao kupitia kwa Aziz Ki kwa mkwaju wa penati baadae Joseph Guede kupachika bao la pili akipokea pasi nzuri kutoka kwa Khalid Aucho.
Hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0, licha ya Simba kuonekana kuongoza kumiliki mpira.
Simba Sc ilipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Freddy Michael na kufanya matokeo kuwa 2-1 ndani ya dakika 90 ya mchezo.