Mkataba wa Tanesco, Songas watakiwa bungeni

WAKATI mkataba wa Ununuzi wa Umeme kati ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Kampuni ya kuzalisha umeme -SONGAS ukitarajiwa kufikia ukomo tarehe 31 Julai, 2024, wabunge wameitaka Serikali kuwasilisha bungeni nyongeza ya mkataba huo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

 Hayo yamebainishwa leo Jumatatu bungeni jijini Dodoma na Mbunge wa Viti Maalum, Jesca Kishoa ambaye katika swali la msingi alihoji makubaliano ya mkataba ujao kati ya Songas na Serikali yamefikia hatua gani.

Jesca Kishoa

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema kwa sasa, Serikali imeunda Timu ya Wataalam (Government Negociation Team – GNT) iliyoanza majadiliano mwezi Aprili 2023 na inatarajia kukamilisha majadiliano hayo kabla ya mkataba kuisha.

“Serikali itahakikisha maslahi ya Taifa yanazingatiwa kabla ya makubaliano yatakayofuata,” amesema.

Aidha, amesema kwa kuwa majadiliano yalianza Disemba mwaka jana pamoja na uweledi wa timu hiyo, wizara itahakikisha hakuna makosa yanayorejewa katika nyongeza ya mkataba huo.

Pia amesema kwa kuwa bado hawajafikia muafaka kwamba Songas wataendelea na mkataba au lah, iwapo wakiendelea serikali itawajibika kuuweka wazi mkataba huo kulingana na sheria za sekta hiyo ya uziduaji.

Related Posts