Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Wateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema kubwa kimaisha baada ya kujumuishwa katika mfumo rasmi wa fedha na taasisi hiyo kupitia kampeni yake ya “NMB Pesa Haachwi Mtu”. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Matumaini hayo kwanza yanatokana na kuweza kufungua akaunti ya NMB Pesa kidijitali kigezo kikubwa kikiwa ni ada ya Sh1000 tu na kitambulisho cha taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa (wapili kulia) akimkabidhi kadi ya pikipiki mshindi wa Pikipiki kwenye uzinduzi wa NMB Pesa Zanzibar, Suleiman Hamad Omari (kulia) katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Kibanda Maiti. Kushoto ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na wapili kushoto ni mkuu wa idara ya mauzo na mtandao wa matawi wa Benki hiyo, Donatus Richard.

Mbali na faida nyingine lukuki za huduma hiyo mpya sokoni, urahisi na nafuu hiyo ni miongoni mwa sababu kubwa zilizowafanya Wazanzibari wengi Jumamosi kufurika katika Viwanja vya Kibanda Maiti kupata fursa ya kuwa na akaunti ya benki kwa mara ya kwanza maishani mwao.

Wakizungumza na waandishi wa habari baada na kabla ya kufungua akaunti zao, wananchi hao pia walisema kivutio kingine kilikuwa ni tamasha lililoambatana na uzinduzi wa kampeni ya “NMB Pesa Haachwi Mtu” Zanzibar.

Kampeni za kuwahamasisha na kuwawezesha watu kunufaika na faida za kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa fedha tayari zimefanyika Kanda ya Dar es Salaam, na Mwanza kwa ajili ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

“Haya ni maendeleo makubwa na kwa utaratibu huu naona nikifika mbali kiuchumi na NMB huku nikiwa na uhakika na usalama wa akiba zangu.

“Hii ni mara yangu ya kwanza kuwa na akaunti ya benki na imetokana na kutokuwepo na mambo mengi kuwa na NMB Pesa kama vile barua ya mjumbe na kadharika,”  alisema Naifat Mohamed Omar ambaye ni mjasiriamali.

Omar Hussein Shemambe naye alisema mikopo hiyo ni kitu kikubwa amevutiwa na kuweza kukopa na kurejesha bila kumhusisha mtu yeyote wala kutembelea tawi la NMB.

“Mimi naona maisha yangu yakienda kubalishwa na NMB kupitia vitu kama hivi. Awali wengi tulikwazwa na mchakato wa kufungua akaunti kuwa mrefu na mambo mengi lakini utaratibu huu mpya ni rafiki sana,” alieleza mkazi huyo wa Bega Moja.

Mzee Kombo Machano alifika kwanza kudhibitisha kama yale ambayo amekuwa akiyasikia kuhusu NMB Pesa Akaunti ni ya kweli hasa kuifunguan kwa TZS 1,000 tena kwa muda mfupi.

Kama walivyokuwa wateja wengine wapya wa NMB waliopatikana siku hiyo, Mzee Kombo amewataka Watanzania kuwa na NMB Pesa Akaunti ambayo pamoja na kutokowa na makato ya kila mwezi lakini pia ni fursa ya kutuma pesa bila gharama yoyote.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa, alisema suluhisho la NMB Pesa ni ushahidi mwingine wa ushiriki wa benki hiyo katika jitihada za kuyaboresha maisha ya Watanzania na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.

“Nawasihi ndugu zangu wa Kibanda Maiti, Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kuichangamkia hii fursa ambayo inaziongezea thamani juhudi za Rais Hussein Mwinyi pamoja na azma ya Rais Samia Suluhu Hassan, za kuwakwamua wananchi kiuchumi na kutokomeza umaskini nchini.”

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema faida za NMB Pesa zina manufaa makubwa hasa kwa wananchi wa kawaida hususani wajasirimali kama mama ntilie na boda boda ambao wanahitaji mikopo rahisi kama Mshiko Fasta ambayo haihitaji dhamana ya aina yoyote.

Related Posts