Mdhamini mkuu wa Ligi ya Vijana chini ya miaka 20
(U20 Youth League) Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi kombe la
ubingwa wa ligi hiyo kwa timu ya Kagera Sugar FC yenye maskani yake
mkoani Kagera baada ya timu hiyo kuibuka bingwa wa ligi hiyo kwa msimu
wa 2023/2024 kufuatia ushindi wake wa penati 3-2 dhidi ya wenzao Dodoma
Jiji FC (U20).
Hafla ya kukabidhi
kombe la ubingwa huo ilifanyika jana
katika uwanja wa Chamazi Complex jijini
Dar es Salaam ikihusisha ushindani mkubwa baina
ya timu hizo mbili hali iliyosababisha hadi dakika 90
zinakamilika matokeo yakiwa 0-0 na hata zilipoongezwa dakika nyingine 30 bado
matokeo yalibakia kuwa hivyo hivyo na hatimaye mshindi kuamuliwa kwa njia penati.
Mkurugenzi wa Hazina
na Masoko ya Fedha wa Benki ya NBC Bw Peter Nalitolela aliiwakilisha benki hiyo
kwenye tukio hilo lililopambwa na uwepo wa mashabiki na wadau mbalimbali wa
mchezo huo wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Wallace Karia.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Nalitolela alisema tukio hilo limehitimisha utoaji
vikombe
vya ligi zote tatu zinazodhaminiwa na benki hiyo kwa msimu 2023/2024
ambapo tayari benki hiyo ilianza
kwa kukabidhi kikombe cha cha Ligi ya Championship kwa timu ya Kengold
ya
mkoani Mbeya mapema mwezi huu huku makabidhiano ya kikombe kingine
yakiwa ni yale
yaliyofanyika mwishoni mwa wiki ambapo ilishuhudiwa benki hiyo ikitumia
helkopta
kuleta kikombe cha Ligi Kuu ya NBC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa
jijini Dar es Salaam kabla ya kukabidhi kwa mabingwa wa ligi hiyo timu
ya Yanga SC yenye maskani yake mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam.
“Kimsingi
tunawapongeza sana vijana wa Kagera Sugar (U20) kwa mafanikio haya na hivyo
wanaungana na mabingwa wengine wawili ambao tayari wamefamikiwa kutwaa vikombe
hivi vya NBC kwa msimu wa 2023/2024. Msukumo wa NBC kudhamini ligi hii ya vijana
unachagizwa na dhamira yetu ya kuwa na ligi kuu yenye ubora na ushindani
kutokana na vipaji vinavyozalishwa hapa nchini.’’
“Umuhimu wa uzalishaji
wa vipaji hivi unaonekana pia hata kwenye timu ya taifa. Hivyo huu ni mwanzo tu
tutaendelea kuboresha zaidi udhamini wetu ili kupata matunda mazuri zaidi,’’
alisema Nalitolela.
Zaidi
Nalitolela alibainisha
kuwa kukamilika kwa ligi hizi kunatoa fursa kwa benki hiyo kuendeleza
programu
zake nyingine za michezo ikiwemo kliniki yake ya vipaji kwa watoto
wadogo inayotambulika kama NBC Football Kliniki sambamba na maandalizi
ya mbio za NBC Dodoma Marathon
zinazotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni zikiwa na lengo la kukusanya
fedha kwa
ajili kusaidia matibabu na upimaji wa saratani ya shingo ya uzazi kwa
wananawake sambamba na kufadhili masomo ya wakunga hapa nchini.
Akizungumzia baadhi ya
mafanikio ya udhamini wa benki hiyo kwenye ligi hizo, Nalitolela alisema umeambatana
na matokeo chanya hata nje mchezo husika
ambapo kupitia mnyororo wa sekta
ya mchezo benki hiyo imeweza kuzalisha ajira za takribani 7,000 kupitia
udhamini huo.
Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (Katikati) sambamba na wadau
wengine wa mchezo wa soka akiwemo Mkurugenzi wa Hazina na Masoko ya Fedha wa
Benki ya NBC Bw Peter Nalitolela (wa tatu kushoto) wakikabidhi kombe la Ligi Vijana
U20 kwa nahodha wa timu ya Kagera Sugar FC (U20) baada ya timu hiyo kuwa bingwa
wa ligi hiyo kwa msimu wa 2023/2024. Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo
ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi
Complex jijini Dar es Salaam ambapo
ilishuhudiwa mabingwa hao wakishinda kwa mikwaju ya penati 3 -2 dhidi ya wenzao
wa Dodoma jijini. Benki ya NBC ni mdhamini mkuu wa ligi hiyo.
Wachezaji wa Kagera
Sugar FC (U20) wakiwa wametulia ka kombe lao baada ya timu hiyo kuwa bingwa wa
Ligi ya Vijana (U20) kwa msimu wa 2023/2024. Hafla ya kukabidhi kombe la
ubingwa huo ilifanyika jana katika
uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es
Salaam ambapo ilishuhudiwa mabingwa hao wakishinda kwa mikwaju ya penati 3 -2
dhidi ya wenzao wa Dodoma jijini. Benki ya NBC ni mdhamini mkuu wa ligi hiyo.
Kikosi cha Dodoma Jiji
FC (U20) kilichoanza kwenye fainali hiyo.
Kikosi cha Kagera
Sugar FC (U20) kilichoanza kwenye fainali hiyo.
Hafla ya kukabidhi
kombe la ubingwa huo ilifanyika jana
katika uwanja wa Chamazi Complex jijini
Dar es Salaam ambapo ilishuhudiwa mabingwa hao wakishinda kwa mikwaju ya penati
3 -2 dhidi ya wenzao wa Dodoma jijini
Baadhi ya maofisa wa
benki ya NBC wakiongozwa na Meneja Masoko wa benki hiyo Alina Kimaryo (katikati)
wakifuatilia fainali hiyo.
Mkurugenzi wa Hazina
na Masoko ya Fedha wa Benki ya NBC Bw Peter Nalitolela (katikati) sambamba na
maofisa wengine wa benki hiyo wakijipongeza kwa kufanikisha maandalizi ya hafla
ya kukabidhi kombe kwa mshindi wa Ligi ya Vijana (U20)
kwa msimu wa 2023/2024. Hafla
ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa
Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ambapo ilishuhudiwa
mabingwa hao wakishinda kwa mikwaju ya penati 3 -2 dhidi ya wenzao wa
Dodoma
jijini. Benki ya NBC ni
mdhamini mkuu wa ligi hiyo.
Muonekano wa kombe
walilokabidhiwa mabingwa hao kama lilivyotolewa na mdhamini wa ligi hiyo benki
ya NBC.
Mkurugenzi wa Hazina
na Masoko ya Fedha wa Benki ya NBC Bw Peter Nalitolela (wa tatu kulia) akiwapongeza
wachezaji wa Kagera Sugar FC (U20) baada
ya timu hiyo kuwa bingwa wa Ligi ya Vijana (U20) kwa msimu wa 2023/2024. Hafla
ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika
jana katika uwanja wa Chamazi Complex
jijini Dar es Salaam ambapo ilishuhudiwa mabingwa hao wakishinda kwa
mikwaju ya penati 3 -2 dhidi ya wenzao wa Dodoma jijini. Benki ya NBC ni
mdhamini mkuu wa ligi hiyo.