BARABARA YA NYENGEDI-RONDO KUJENGEWA KWA KIWANGO CHA LAMI,KIONGOZI WA MWENGE MNZAVA AWEKA JIWE LA MSINGI


Na Elizabeth Msagula Lindi,

Wananchi wa kijiji cha Mkangambili na Nyengedi halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi wamefurahishwa kwa hatua ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Nyengedi-Mnara -Rondo yenye urefu wa km 1.15 kwa kiwango cha lami .

Wakazi hao wamesema barabara hiyo itakapokamikika itawasaidia kuunganisha mawasiliano kati ya wananchi wa Nyengedi na Rondo na pia kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo hususan mazao.

“Kabla ya hapo adha ilikuwa kuwa hasa kwenye kusafirisha mazao yetu kutoka mashambani lakini wajawazito walikuwa walikuwa wanateseka kufika kituo cha afya kwa sababu barabara ilikuwa korofi sana na wa mama wengine walikuwa wanajigungulia njiani “Alisema Ramadhan Selemani Nchia Mkazi wa Kijiji cha Mkangambili -Rondo.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa kwa mwaka 2024 Godfrey Mnzava ameweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara hiyo Mei 27,2024 inayogharimu Kiasi cha shilingi 939,107 ,800.00 ikiwa ni utekelezaji wa adhma ya Serikali ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa halmashauri ya Mtama na hivyo kupunguza gharama za matengenezo ya kila mwaka.

Kabla ya kuweka jiwe la msingi kiongozi huyo wa Mwenge wa uhuru Kitaifa Mnzava ameeleza matumaini yake juu ya mradi huo kuwa utakamilika kwa wakati uliopangwa mwezi Oktoba Kama mkataba unavyoelekeza huku akiwahimiza Wakala wa barabara za mijini na Vijijini Tarura kusimamia vizuri ili wanachi wapate unafuu wa huduma ambazo zitategemea barabara hiyo.

Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa (TARURA)Wilaya ya Lindi Mhandisi Dawson Paschal amesema mradi unatekelezwa naa Mkandarasi M/s.M.E & Company Limited ukiwa kwa sasa umefikia asilimia 15 ya utekelezaji na unakwenda kukamilisha urefu wa km 7.1 ambazo zinajengwa kwa sehemu tofauti zilizokuwa korofi zaidi.

Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2024 ukiwa katika halmashauri ya Mtama umekimbizwa kwa umbali wa Km 204.2 ukipita katika miradi 8 ya maendeleo yenye thamani ya Bilion 2.526 .

Related Posts