MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umewataka watetezi wa haki za Binadamu kwa jamii ya wafugaji kuongeza juhudi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuwa hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezi watetezi hao yaliyofanyika mkoani Arusha.
Olengurumwa aliwataka watetezi wa haki za wafugaji kushikamana ili waweze kulitetea kundi hilo changamoto zao zitatuliwe.
“Sekta ya ufugaji ni ya pili kwa kuchangia maendeleo ya taifa na insaidia kupatikana chakula hivyo ni muhimu kwa maendeleo inabidi ilindwe,” alisema Olengurumwa.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Mrinda Mshota alisema chama chake kinaendelea kuwaunganisha wafugaji ili kuangalia namna ya kutatua changamoto zao.
Aidha, Mshota aliiomba Serikali kufanya majadiliano na wafugaji walioko karibu na Hifadhi ya Ngorongoro, kuangalia namna ya kutekeleza zoezi la kuwahamisha bila kukiuka haki zao kwa kuwa suala hilo ni mtambuka.