Nicki Minaj atangaza tarehe mpya ya show yake baada ya kukamatwa kwenye uwanja wa ndege

Baada ya kulazimishwa kughairi onyesho lake wikendi iliyopita kufuatia kukamatwa kwake na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Amsterdam Schiphol, rapa Nicki Minaj alitangaza tarehe  mpya iliyopangwa tena kwaajili ya tamasha lake la Pink Friday 2 Tour.

Akitumia mtandao wake wa kijamii Jumatatu, Mei 27, hitmaker huyo wa Anaconda alitangaza kuwa onyesho hilo ambalo awali lilipaswa kufanyika Mei 25 sasa litafanyika Juni 3 katika ukumbi huo huo wa Co-op Live.

Akifafanua uamuzi huo, aliandika, “ok, watu wangu, nilishauriwa TENA kwamba HATUWEZI kufanya tarehe nyingine yoyote kwa tarehe ya #gagcityMANCHESTER tofauti na ya JUNE 3.”

Related Posts