Kenya yafanya mikutano ya hujuma ya wanajeshi wa Uingereza – DW – 28.05.2024

Vikao hivyo vitakavyofanyika hadi Alhamisi wiki hii, vitachunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mateso, kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria na hata mauaji.

Bunge la Kenya wiki iliyopita lilitangaza kuwa litafanya mikutano minne ya umma, ukiwemo mmoja utakaofanyika mjini Nanyuki, juu ya madai ya dhuluma zilizofanywa na wanajeshi wa Uingereza nchini humo.

Kambi ya mafunzo ya jeshi la Uingereza nchini Kenya ni moja kati ya tegemeo la kiuchumi kwa wakaazi wengi mjini Nanyuki japo wanajeshi wa Uingereza katika kambi hiyo wameshutumiwa kufanya hujuma mbalimbali dhidi ya wenyeji, yakiwemo mauaji.

Kuuwawa kwa mazingira tata ya Agnes Wanjiru

Katika kisa kilichotazamwa kwa uzito wa juu cha mwaka wa 2012, mwili wa mwanamke wa umri mdogo wa Kikenya ulikutwa kwenye tanki la maji taka huko Nanyuki ambapo mara ya mwisho alionekana akiwa hai pamoja na mwanajeshi wa Uingereza.

Familia ya Agnes Wanjiru ilifungua kesei huko Kenya kuhusu kifo cha mama huyo aliyekuwa na umri wa miaka 21, lakini maendeleo yamekuwa ya kusuasua, huku kesi zikiahirishwa mara kwa mara. Kesi hiyo sasa inatazamiwa kusikizwa Julai 10, kwa mujibu wa  vyombo vya habari vya ndani.

Kenya |   Kitengo cha Mafunzo ya Jeshi la Uingereza nchini Kenya (BATUK)
Wanajeshi ambao ni sehemu ya kikundi cha mafunzo kinachojumuishwa katika hifadhi ya Loldaiga huko Laikipia, chini ya Mlima Kenya., Novemba 14, 2022.Picha: THOMAS MUKOYA/AFP

Pamoja na mateso mengine yalioanishwa vikao hivyo pia vitachunguza madai ya ukiukaji wa kimaadili unaohusiana na utovu wa nidhamu, ikiwa ni pamoja na rushwa, ulaghai, ubaguzi, matumizi mabaya ya mamlaka na tabia nyingine zisizo za kimaadili.

Tofuati ya masuala ya usalama kati ya Kenya na Uingereza

Serikali za Uingereza na Kenya zimekuwa katika mzozo kuhusu suala la mamlaka ya wanajeshi wa Uingereza wanaovunja sheria za Kenya, huku serikali ya Uingereza ikisema hapo awali kwamba haikukubali mamlaka ya mahakama ya Kenya kuchunguza kifo cha Wanjiru.

Alipoulizwa kuhusu vikao vya wiki hii, msemaji wa Ubalozi wa Uingereza aliiambia AFP: “Ubalozi wa Uingereza mjini Nairobi na BATUK wanakusudia kushirikiana na uchunguzi huo.”

Zaidi alisema “Ushirikiano wa ulinzi kati ya Uingereza na Kenya ni mojawapo ya nguvu kuu za uhusiano wetu na mafunzo na operesheni zetu za pamoja na jeshi la Kenya kwa lengo la  salama wetu.”

Mwakilishi wa Uingereza alikutana na familia ya marehemu

Siku ya Alhamisi, ujumbe wa Uingereza ulisema Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Neil Wigan alikutana na familia ya Wanjiru, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikidai haki kuhusu mauaji yake.

Ikumbukwe tu, Oktoba 2021, gazeti la The Sunday Times la Uingereza liliripoti kwamba mwanajeshi mmoja alikiri kwa wenzake kumuua Wanjiru na kuwaonyesha mwili wake. Ripoti hiyo ilidai kuwa wakuu wa jeshi walifahamishwa kuhusu mauaji hayo, lakini hakuna hatua zaidi zilizochukuliwa.

Chanzo: Biden, Ruto kujadili msamaha wa deni kwa Kenya wiki hii

Mwaka 2019 kulianzishwa uchungu lakini hakuna matokeo ambayo yametolewa kwa umma.Polisiwa Kenya kwa upande wao walitangaza kuwa uchunguzi wao utaanzishwa tena baada ya ufichuzi wa taarifa za gazeti la Sunday Times.

Chanzo: AFP

Related Posts