Wakazi 12 wa Ifakara-Morogoro wafikishwa mahakamani kwa kuongoza genge la uhalifu kujipatia pesa

Wakazi 12 wa Ifakara mkoa wa Morogoro wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiwemo Barnaba Gidajuri (45) wakikabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu na kujipatia pesa shilingi millioni 10 kwa njia ya udanganyifu.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Ushindi Swalo ambapo Wakili wa Serikali Tumaini Mafuru alidai watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka thelathini na mbili.

Wakili Mafuru alidai mashtaka hayo ni kuongoza genge la uhalifu waliofanya Januari mosi hadi Mei 5, 2024, ambapo walituma jumbe fupi kwa watu kisha kujipatia kiasi cha Sh millioni 10.

Aidha Wakili Mafuru alidai mashtaka ya pili na ya tatu yanayomkabili mtuhumiwa Barnaba Gidajuri ilitotenda Januari 4, mwaka huu akisambaza jumbe fupi kwa njia ya mtandao wenye maneno “Mzee huyu Mganga wa tiba asili anatoka mali bila kafara, cheo, mapenzi……”..”jiunge na chama huru cha freemason (666) Tanzania bila kutoa kafara ya binadamu…..”

Kwa mujibu wa Wakili mashtaka mengine manne yanayomkabili Barnaba ambapo akiwa Mkoa wa Morogoro mshtakiwa alitumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina tofauti bila ruhusa na idhini ya wamiliki.

Aliendelea kudai kuwa mashtaka ya nane yanayomkabili mtuhumiwa huyo alitenda Mei 11, 2024 kwa kujipatia shilingi 105,000 kutoka kwa Maria Nangwa baada ya kujitambulisha kuwa ni Mganga atakayemtibia ugonjwa wake wa kifafa.
Mahakamani hapo Wakili alidai mashtaka tisa na kumi yanayomkabili mtuhumiwa Rahim Bangila (26), kwa kusambaza jumbe fupi kwa njia ya mtandao wenye maneno.”Mimi mwenye nyumba wako apa mbona siku zinazidi?”

Wakili Mafuru alidai mtuhumiwa Rahim anakabiliwa ni mashtaka matatu kwa kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya Valence Mandaki, Nundu Gulenya na Stephen Lihami bila ruhusa ya watu hao.

Aidha, Wakili alidai mtuhumiwa mwingine Ramadhan Mcheni (28) anakabiliwa na mashtaka mengine mawili ya kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine bila ruhusa yao.
Ilidaiwa Mahakamani hapo mashataka mengine mawili yanayomkabili mtuhumiwa Leonard Mwilenga (23), ambapo Mei 6, mwaka huu alitumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine bila ruhusa yao.

Hata hivyo, Wakili aliendelea kudai Mashtaka mawili mengine yanamkabili mtuhumiwa Mohamed Masalanga (24), ambaye alitumia laini ya Irene Said bila idhini yake.

Aidha mashtaka mengine ni kusambaza jumbe fupi tofauti kwa njia ya mtandao na kujipatia kiasi cha shilingi 389,000 benki ya CRDB kwenda kwa Odilia Mathew kinyume na sheria”habari ya leo mimi mwenye nyumba wako mbona kimya na siku zinaenda?”…..umepokea kiasi cha shilingi…..”, pia kutumia laini yenye usajili wa mtu mwingine bila idhini yao.

Pia mashtaka mengine yanamkabili mtuhumiwa Noel Noel Mboya (37) @Mkono wa chuma, ni kosa la kuharibu na kupoteza ushahidi kwa kuharibu simu aina ya Tecno na kupoteza uhalisia wa simu hiyo na kufanya ushahidi usionekane.

Wakili alidai mashtaka mengine yanayowakabili washtakiwa ni kujipatia pesa shilingi milioni 10 kwa njia ya udanyanyifu kutoka kwa watu tofauti kuwa pesa hizo zimetumwa kimakosa katika simu zao hivyo zirudishwe.

Katika mashtaka ya mwisho washtakiwa wote kwa pamoja anashtakiwa kwa kosa la utakatishaji fedha, ilidaiwa kuwa washtakiwa walijipatia Sh millioni10 wakijua pesa hizo ni madharia ya mashtaka ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka yao washtakiwa hakutakiwa kujibu kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo. Washtakiwa walirudishwa rumande kutokana kesi yao kutokuwa na dhamana.

Kesi hiyo ilihairishwa hadi June11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi bado unaendelea.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Rahim Bangila ( 20), Ramadhan Mcheni (28, Leonard Mwilenga (23), Mohamed Masalanga (24), Festo Ndizi(27), Richard Masunga (23), Zabron Mkoi (22), Noel Mboya@mkono wa chuma(37), Shafii Mtambo (18), Musa Lwena(23) na Agrey Razaki (23) wote wakiwa ni wakazi wa Ifakara Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 15, mwaka huu na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, ilisema watuhumiwa hao walikuwa wakipiga simu na kusambaza jumbe fupi za maneno (sms) wakidai pesa inatumwa kimakosa hivyo irudishwe, wengine wanadai kusafisha nyota, ilikupata utajiri……, wengine kujifanya Maofisa wa Serikali kwa kudai kwamba watatatua shida za watumishi wenye matatizo na mwisho huishia kuwaibia watu pesa kwa njia ya mtandao.

Katika msako huo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata washtakiwa wakiwa na simu 41 na laini za simu 88 za mitandao tofauti zikiwa na usajili tofauti tofauti.

Related Posts