IGP WAMBURA AKUTANA NA RC MTAKA

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka wakati alipomtembelea ofisini kwake leo Mei 28,2024 ambapo waliweza kujadiliana masuala mbalimbali hususani eneo la usalama katika Mkoa huo wa Njombe.


IGP Wambura amefanya ziara ya kikazi mkoani humo na kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo jengo la ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe pamoja na kuzungumza na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali na kuwakumbusha juu ya umuhimu wa kutenda haki kwa wananchi, kutoa huduma bora, kuzingatia maadili na weledi muda wote wanapotekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.




Related Posts