ATE, TUCTA, VETA Kuimarisha ujuzi Wahitimu wa Mafunzo ya Ufundi

Mtendaji Mkuu wa Chama  cha waajiri Tanzania (ATE) Suzanne Ndomba Doran na Katibu Mkuu wa Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Herny Nkunda wakisaini mikataba na  mikataba waliyosaini kwaajili ya kuimarisha Mafunzo ya Ufundi.

Mtendaji Mkuu wa Chama  cha waajiri Tanzania (ATE) Suzanne Ndomba Doran akizungumza wakati wa utiaji wa saini ya kutekeleza makubaliano ya Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Shirikisho la wenye viwanda (CTI), Vyuo vya ufundi Stadi (VETA) na Sekta mbalimbali nchini wamesaini mkataba wa makubaliano kuendeleza mafunzo ya ujuzi kwa wanafunzi wanaohitimu masomo yao ili waweze kujiari au kuajiriwa.

Katibu Mkuu wa Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Herny Nkunda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya utiaji wa saini ya kutekeleza makubaliano ya ATE, Shirikisho la wenye viwanda (CTI), Vyuo vya ufundi Stadi (VETA) na Sekta mbalimbali nchini wamesaini mkataba wa makubaliano kuendeleza mafunzo ya ujuzi kwa wanafunzi wanaohitimu masomo yao ili waweze kujiari au kuajiriwa.

Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

CHAMA cha waajiri Tanzania (ATE), Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Shirikisho la wenye viwanda (CTI), Vyuo vya ufundi Stadi (VETA) na Sekta mbalimbali nchini wamesaini mkataba wa makubaliano kuendeleza mafunzo ya ujuzi kwa wanafunzi wanaohitimu masomo yao ili waweze kujiari au kuajiriwa.

Akizungumza leo, Mei 28, 2024, wakati wa utiaji wa saini ya kutekeleza makubaliano hayo Mtendaji Mkuu wa ATE, Suzanne Ndomba Doran amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidi wanafunzi kupata mafunzo ya amari baada ya kumaliza nadharia waliyoipata darasani.

“Leo Tumesaini mkataba baina yetu ATE pamoja na shirikisho la wenye viwanda CTI na vyama vya wafanyakazi (TUCTA), vyuo vya Ufundi, Umoja wa Walima Chai na Umoja wa mahoteli pamoja na umoja wa wajiri na wafanyakazi wa Denmark.

“Tukiwa kama chama cha waajiri tunaziunganisha Sekta tofauti, tumesaini makubaliano na vyama vya wafanyakazi ambapo tumekuwa tukifanya nao mradi wa miaka mitatu wa kuendeleza ujuzi pahala pa kazi”. Amesema Suzan.

Amesema kuwa wamesaini mkataba huo na vyuo vya ufundi vilivyo chini ya VETA na mradi huo utajikita kwenye ujuzi wa Fitter Mechanics, Domestic and Industrial , Electrical Installation, Food Production , Hotel Management, Bekery and Refrigeration na air Condition (cooling).

“Katika kipindi kilichopita tulianza kufanya miradi yetu mwaka 2021 Juni katika mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro katika eneo la Donbosco VTC, Mzinga, kihonda VTC, Veta Dar es Salaam….lengo la mradi ni kuhakikisha tunapunguza gape ya ujuzi (ombwe la vijana kutokuwa na ujuzi ) ili waweze kujiajiri wenyewe lakini pia weweze kuajiriwa”.

Suzanne amesema kuwa vijana hao wanapatikana kupitia matangazo yanayotelewa kwenye vyuo mbalimbali vya ufundi na kwamba mafunzo hayo yanawasaidia wanafunzi kupata ujuzi zaidi kutoka kwenye nadharia wanayofundishwa vyuoni na kupata ujuzi wa vitendo.

Amesema mpaka sasa wanafunzi 1006 wamenufaika katika awamu tatu huku walimu wakiwa 19 kampuni 57 zilishiriki na kusaini mkataba wa kuchukua wanafunzi kwa ajili ya mafunzo ya vitendo.

“Awamu ya kwanza tulikuwa na wanafunzi 277 ambapo wanafunzi 270 walifanikiwa, wamu ya pili tulikuwa na wanafunzi 436 ambapo wanafunzi 324 walifanikiwa, na awamu ya tatu tulipata wanafunzi 300 “

“Tumefanikiwa kutoa (skills study) ujuzi ili vijana wame ili wajiajiri au vijana wetu wawezr kupata nafasi kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati ya kinchi”

Amesema kuwa mradi huo umesaidi kuwapa nafasi wanawake ili kuendelea kumnyanya mwanamke.

Amesema kwa kuwa Teknolojia inabadilika na kunakuja Teknolojia mpya anaamini ushirikiano huo utawafanya vijana kuendana na teknolojia hiyo kwa kuwa mara nyingi ujuzi huo huanzia sehemu za ajira kabla kufika katika vyuo.

Kwa upande wake, Herny Nkunda Katibu Mkuu wa Tucta, amesema mradi huo utaboresha ujuzi wa wafanyakazi na wanafunzi .

“Wanafunzi baada ya kuhitimu mafunzo yao uwezo wao ulikuwa mdogo waajiri wengi walikuwa hawapati kile walichotegemea kutoka kwa wanafunzi wanapotoka kwenye mafunzo sisi tulipogundua hilo tukakaa pamoja na waajiri kuweza kujua mahitaji yao baada ya kujua mahitaji yao tukakaa na wenzetu wa Veta kupitia NacteVet tukatengenez mitaala ambayo ilikuwa inaziba mianya iliyoonekana kwa wanafunzi waliohitimu na kuingia sokoni tukaamua kuwafundisha walimu wa veta kama mnavyoona sasa wanafunzi kadhaa washahitimu.

Amesema mradi huo umewanufaisha waajiri kwa kupata vijana wenye ujuzi na ajira kuongezeka pamoja na uzalishaju utaongezeka.

Mtendaji Mkuu wa Chama  cha waajiri Tanzania (ATE) Suzanne Ndomba Doran na Katibu Mkuu wa Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Herny Nkunda wakionesha mikataba waliyosaini kwaajili ya kuimarisha Mafunzo ya Ufundi.

Baadhi ya washiriki.

Related Posts