Uchaguzi wa Viongozi wa CHADEMA Kanda ya Nyasa unafanyika leo May 29,2024 katika Mji wa Makambako Mkoa wa Njombe kwa kushuhudia Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ akimbwaga mpinzani wake kwa tofauti ya kura mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Katika uchaguzi uliofanyika leo Jumatano kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria wa Neema – Makambambo mkoani Njombe, Sugu amepata kura 54 ilihali Msigwa akivuna kura 52.
Vigogo hao wawili wamechuana kupata Uenyekiti wa Kanda hiyo ambao mshindi ni Joseph Mbilinyi (SUGU) huku Mchungaji Msigwa akishindwa kutetea kiti chake.
Katika uchaguzi huo uliofanyika jumla ya wajumbe 109 kutoka majimbo 31 wameshiriki kupiga kura kuchagua viongozi wao.
Awali Katibu wa Kanda ya Nyasa, Gwamaka Mbughi alisema mpaka hakuna Mgombea aliyejitoa na wote wameshafika Makambako na uchaguzi huo umeanza ukisimamiwa na Naibu Katibu Mkuu Bara Benson Kigaila.
Kanda hiyo ndiyo imeonekana kuwa na ushindani mkubwa kuliko kanda zingine na kulikuwa na kupigana ‘vikumbo’ vya hapa na pale miongoni mwa vigogo hao machachari wa CHADEMA pamoja na wafuasi wanaowaunga mkono kila upande ukitumia mbinu kujigamba.