Ishu ya Hamisa Mobetto, Azizi Ki iko hivi

MWANAMITINDO na mwanamuziki, Hamisa Mobetto amefafanua kuhusu ukaribu wake na mchezaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki na kuzungumzia pia uvumi kwamba ana uhusiano na kigogo wa soka ambaye yupo karibu na mshindi huyo wa tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara 2023-24.

Akizungumza na Mwanaspoti, Hamisa Mobetto amesema hana uhusiano na kigogo yeyote wa soka na pia wala Azizi Ki si mpenziwe kama baadhi ya watu wanavyodhani, akisisitiza nyota huyo wa boli ni rafiki yake na anamshabikia japo yeye ni shabiki wa timu ya Simba.

“Sina uhusiano na bosi yeyote, mimi kwa sasa nipo single, Azizi Ki ni rafiki yangu na nakubali kazi yake anapambana, mimi timu yangu ni Simba.”

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Hamisa alijumuika na wachezaji wa Yanga waliokuwa wakishangilia kukabidhiwa kombe la ubingwa wa tatu mfululizo wa Ligi Kuu Bara katikati ya Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kumalizika kwa mechi ya ligi dhidi ya Tanzania Prisons Jumanne iliyopita na akaonekana akimfuta kitu usoni Aziz Ki aliyekuwa kwenye kilele cha furaha ya ubingwa.

“Ila watu wako hivyo, wakiniona na mtu karibu wanaanza kuniunganishia matukio, zamani nilikuwa nikiona hivyo nakuwa mnyonge lakini kwasasa nishazoea wala hawanistui kabisa,” alisema Hamisa.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Aidha, Hamisa Mobetto amedai kwamba yeye si mwanamke anayependa wanaume wenye uwezo mkubwa kifedha kama tuhuma dhidi yake zinavyosambazwa.

“Mimi napenda mwanaume anayejielewa, mwenye upendo na watoto wangu na awe na huruma juu ya mapenzi, ikitokea ana fedha itakuwa imetokea, lakini si mwanamke ninayependa pesa kuliko utu na mapenzi ya kweli,” alisema na kuongeza:

“Unajua mimi ni mama wa watoto wa wiwili, sasa nikisema kwenye uhusiano niangalie tu pesa bila upendo kwa watoto wangu itakuwa kazi bure, yaani inatakiwa mwanaume apende boga na ua lake, pesa sio kikwazo katika maisha yangu, kwa sababu najua kuitafuta hivyo siwezi kubweteka kwa kutaka mwanaume mwenye pesa, hilo kwangu halipo.”

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Aidha, Hamisa alisema alipojitambua na kuachana na masuala ya mapenzi amejiona amechelewa kufanya uamuzi baada ya riziki kuanza kufunguka hasa kupata tenda za ubalozi katika kampuni tofauti.

Mwanadada huyo amezaa mtoto wa kwanza na bosi wa EFM Radio na TV, Majizo na mtoto wa pili akitajwa kuzaa na supastaa wa Bongofleva, Diamond Platnumz, huku pia akiwa na ukaribu na rapa tajiri wa Marekani, Rick Ross.

Related Posts