Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
KATIBU Tawala wa wilaya ya Same, Upendo Wella nidhamu ni jambo la msingi katika michezo, hivyo amewaombe wanafunzi ambao wanakwenda kushiriki mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Sekondari Tanzania(UMISETA) kuheshimu kila mtu.
Ameyasema hayo hayo alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Same Kaslida Mgeni kwenye kuhitimisha Umoja wa Michezo na Taaluma shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) ambapo amewaomba pia wanafunzi ambao wanashiriki Mashindano hayo kuendelea kujikita zaidi kwenye masomo ili kutimiza ndoto zao.
Amesema kutimizwa kwa ndoto za wanafunzi hao kunakwenda kuleta maslahi mapana ya Taifa huku akifafanua michezo inaambatana na elimu.
“Unakuta sasa hivi baadhi ya vijana wengi ambao wanashiriki kwenye michezo mbalimbali wamepata mafanikio makubwa,”amesema na kuwasisitizia walimu, wafanyakazi, na wanafunzi kudumisha na kuendeleza michezo, maana michezo ni afya.
“Pia michezo ni ajira lakini inadumisha mahusiano mazuri kwa vijana wetu. Hivyo, michezo inaleta maendeleo makubwa katika Taifa letu. Ndiyo maana tunamuona Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, anavyotoa hamasa kubwa kwa timu zetu hapa nchini kwenye mashindano tofauti ndani na nje ya nchi.”