Watu 36 waliwa na mamba Buchosa

MBUNGE wa Buchosa mkoani Mwanza, Eric Shigongo ameiomba Serikali kuchukua hatua za dharura kuokoa maisha ya wananchi wa wilaya hiyo hasa ikizingatiwa jumla ya watu 36 wameuawa na kuliwa na mamba katika kipindi cha miaka mitatu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Amesema mbali na kuwa na majina ya watu wote waliopoteza maisha kutokana na kukithiri kwa Wanyama hao, amesema tukio la hivi karibu limetoka tarehe 14 Aprili mwaka huu ambapo ni la mama mmoja aliwaacha watoto wake wawili nyumba na kwenda kuchota maji kwenye Ziwa Victoria lakini bahati mbaya akaliwa na mamba na kuwaacha watoto hao yatima.

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo

Akiwasilisha hoja ya dharura kwa mujibu wa kanuni ya 54 leo Ijumaa bungeni jijini Dodoma, Shigongo amesema maisha ya Wanyama hao huko Buchosa yamekuwa muhimu kuliko ya binadamu.

“Juzi tulikutana kwenye semina ya maliasili na utalii juu ya wanyama wakali wanavyoshambulia watu ila mamba hakutajwa. Ni kweli kabisa mamba analindwa na sheria za kimataifa, upo mkataba unaitwa CITES unataka mamba alindwe.

“Lakini haki ya kuishi ya binadamu inalindwa na sheria na yapo maazimio ya kimataifa ambayo yanahakikisha haki ya binadamu kuishi inalindwa. Kwa hiyo binadamu lazima aishi kwanza kabla ya mamba kuishi lakini ninachokiona ni kwamba mamba anaanza kuwa na thamani kuliko binadamu wa buchosa. Kwa msingi huo ninaomba sana tutafuta namna ya kujadili kama wabunge ili kuishauri wizara kwamba tutafanya nini kuokoa maisha ya watu,” amewasilisha Shigongo.

Licha ya kuungwa mkono na wabunge, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema pamoja na wabunge kujali kwanza uhai wa binadamu, kwa kuwa bajeti inayoendelea kujadiliwa ni ya wizara ya maliasili na utalii wabunge watumia fursa hiyo kuishauri Serikali nini cha kufanya ili kuokoa wananchi wa Buchosa na maeneo mengine.

Related Posts