Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Oryx Services and Specialties Ltd iliyoendesha shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx leo Mei 31,2024 imekabidhi tiketi kwa washindi wa shindano hao ambao watakwenda Dubai na gharama zote zitagharamiwa na Kampuni hiyo.
Shindano hilo lilianza Januari na kumalizika Desemba 2023 ,hivyo leo wametangaza washindi wawili ambao ni Mbise Oil Shop iliyopo Arusha (Oryx Shop) pamoja na Lwimba Investment Company Ltd iliyopo Dar es salaam (Msambazaji).
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi tiketi kwa washindi hao Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta amesema zawadi ya shindano hilo ni Safari ya kwenda Dubai.
“Washindi wetu wanakabidhiwa tiketi zao tayari kwa safari. Gharama zote za safari hii ya Dubai zimelipiwa na kampuni ya Oryx Services and Specialities Limited. Kila mshindi amepata tiketi mbili kwa ajili ya safari ya Dubai.
“Tunawatakia washindi wetu safari njema na salama. Tunatarajia kutangaza mashindano yafuatayo hivi karibuni ambayo yatakuwa ya kusisimua zaidi kuliko shindano lililopita. Ni matumaini yetu wauzaji wetu wote watashiriki tena vyema kama mwaka uliopita.
“Oryx Energies ni kampuni kubwa na ya muda mrefu ya kimataifa inayotoa huduma za nishati barani Afrika. Oryx Energies huagiza, kuchakata, huhifadhi na kusambaza bidhaa za mafuta ya magari, machine na mitambo (Dizeli, Petroli, Vilainishi) na gesi za kupikia (LPG) zitumikazo katika sekta mbalimbali za uchumi.”
Akieleza kuhusu kampuni hiyo Mehta amesema Oryx Energies ni msambazaji namba moja wa bidhaa za mafuta na vilainishi katika sekta ya uchimbaji madini (migodi) na inaongoza kusambaza vilainishi katika sekta zingine za kiuchumi.
Ametaja sekta hizo za kiuchumi ni usafirishaji wa nchi kavu (pikipiki, magari, treni) na majini, viwandani, ujenzi na kilimo huku akifafanua pia huzalisha na kusambaza vilainishi mbalimbali kuanzia vya magari, mitambo ya migodini na viwandani, uzalishaji wa umeme.
“Kila kilainishi cha Oryx kimetengenezwa kwa uangalifu na kwa ubora wa juu zaidi na timu yetu ya wataalamu nchini Uswizi na kuchanganywa katika Kiwanda cha kipekee kinachotumia teknologia ya kisasa kilichoko Kurasini, Tanzania.
“Maduka ya Kipekee ya Oryx yapo nchini kote na hutoa huduma za kipekee, zinazohakikisha upatikanaji wa bidhaa halisi na huduma bora kwa watumiaji wetu. Katika kuhakikisha bidhaa na huduma zinapatikana kwa watumiaji kote nchini, Oryx Energies inaendelea kuboresha njia zake za usambazaji kwa kupitia Maduka ya Kipekee ya Kampuni (CODOs), Wasambazaji na vituo vya mafuta vya Oryx.
Kwa upande wake Vaileth Cilwimba kutoka Lwimba Investment Company Ltd jijini Dar es salaam (Msambazaji) ambaye ni mmoja wa washindi hao amesema kuendeshwa kwa shindano hilo ni sehemu ya kuongeza hamasa kwa mawakala wa bidhaa za vilainishi vya Oryx na wao wanajivunia kuwa wauzaji bora kupitia shindano hilo.
“Tunashukuru kwa kushinda na kupata tiketi kwa ajili ya kwenda Dubai ambapo tumelipiwa kila kitu kwa maana ya gharama zote, kwetu hii inatufanya tuongezee bidii zaidi kwa kuuza zaidi bidhaa bora za Oryx zikiwemo za Vilainishi vya magari,bodaboda na bajaji.”
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta akimkabidhi mfano wa zawadi ya tiketi ya Safari ya kwenda Dubai Mwakilishi wa Kampuni ya Mbise Oil Shop iliyopo Arusha (Oryx Shop)(Msambazaji) ambaye ni mshindi wa shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx. Zozi la ugawaji wa tiketi hizo limefanyika leo Mei 31,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta akimkabidhi mfano wa zawadi ya tiketi ya Safari ya kwenda Dubai Vaileth Cilwimba kutoka Lwimba Investment Company Ltd jijini Dar es salaam (Msambazaji) ambaye ni mshindi wa shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx. Zozi la ugawaji wa tiketi hizo limefanyika leo Mei 31,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx ambapo washindi hao wamezawadiwa tiketi ya kwenda Dubai. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 31,2024 Jijini Dar es Salaam