DKT.BITEKO AMPONGEZA MBUNGE MAVUNDE KWA KUWEKA  MIKAKATI YA KUINUA ELIMU DODOMA JIJI

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto  Biteko,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la  Dodoma  ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la  Dodoma  ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la  Dodoma  ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la  Dodoma  ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la  Dodoma  ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Naibu  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto  Biteko (hayupo pichani) ,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la  Dodoma  ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto  Biteko,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa Photocopiers 10 kubwa kwa lengo la kuchapisha mitihani na kuwapunguzia mzigo wazazi wa watoto wa Dodoma Jiji kuchangia fedha za mitihani ya majaribio ya kila wiki.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto  Biteko,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la  Dodoma  ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto  Biteko amempongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde kwa ubunifu wa kuandaa mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting wenye lengo la kujadili mikakati ya kuboresha na kukuza Elimu katika jiji la Dodoma.

Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo leo Juni 1,2024  katika mkutano wa walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jijini  Dodoma  ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma mjini, Mhe.Anthony Mavunde.

“Mhe.Mavunde wewe ni shujaa wa wananchi wa Dodoma Mjini nakupongeza kwa ubunifu wako wa hali ya juu leo upa hapa na wakuu wa Shule za Msingi & Sekondari na Waratibu Elimu Kata kwa lengo la kujadiliana changamoto za muhula uliopita na kujipanga na mhula ujao kuanzia mwezi Julai 2024.”amesema Dkt.Biteko

Dkt.Biteko amesema kuwa yeye pamoja na Waziri wa Elimu Prof.Mkenda wamejifunza kutokana ubunifu uliofanywa na  Mhe.Mavunde katika kuweka Mikakati ya kuboresha Elimu kwenye jijini la Dodoma hata sisi tutaenda kufanya katika majimbo yetu.

Aidha Dkt. Biteko  amewaasa walimu nchini kudumisha maadili katika ufundishaji ili kuwaandaa viongozi bora wa siku zijazo ambao hawajapandikizwa mitazamo hasi isiyo na tija kwa maendeleo ya taifa.

“Kama tunataka kujenga taifa lenye ustaarabu, kustahimiliana na lenye amani, mahali pekee pa kuwekeza ni kwenye elimu, mataifa yote yaliyoendelea uwekezaji wake mkubwa upo kwenye elimu”amesisitiza  Dkt. Biteko

Kwa upande wake Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,amempongeza hatua hiyo ya kuwaongezea morali wa kufanya kazi walimu kwa kukutana pamoja na viongozi kujadiliana changamoto za kwenye sekta ya Elimu.

“Serikali inajenga vyuo 64 vya VETA nchi nzima, kampasi za vyuo vikuu kwenye mikoa karibu yote nchini ili kuboresha upatikanaji wa elimu kwenye maeneo jirani.”amesema Prof.Mkenda

Naye ,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde, amesema lengo la kukutana na walimu hawa ni kujadiliana mafanikio na changamoto za mhula  uliopita na kujipanga na mhula ujao ili tuweze kulitendea

haki jiji letu la Dodoma kwenye sekta ya elimu kwa kuweka mikakati kabambe ya kuboresha sekta.

“Tuliona njia pekee ya kufanya vizuri ni kuwaweka walimu pamoja hatutaki mwalimu wetu akiwa na changamoto akalalamike kwani haya  ni sehemu ya maisha yetu,”amesema Mhe. Mavunde

Mhe.Mavunde amesema kupitia Mkutano huo watazungumza kwa pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kutatua kero ambazo zitajitokeza.

“Dhamira yangu ni ya dhati katika kukuza elimu  kwani nimeweza kujenga shule za msingi na sekondari kwa wanafunzi waliokuwa wakitembea umbali mrefu,”amesema Mhe.Mavunde.

Amesema kwa kushirikiana na baadhi ya wadau  wameweza kujenga uzio katika shule mbalimbali  ambao unasaidia watoto kusoma kwa utulivu.

Katika hatua nyingine Mhe. Mavunde amekabidhi Photocopiers 10 kubwa kwa lengo la kuchapisha mitihani na kuwapunguzia mzigo wazazi wa watoto wa Dodoma Jiji kuchangia fedha za mitihani ya majaribio ya kila wiki.

Related Posts