Watu wameokolewa katika vijiji kadhaa vilivyoko pembezoni mwa mto Danube na Schmutter huku afisa mmoja akielezea wasiwasi kuhusiana na kufurika kwa bwawa lililoko eneo hilo.
Kulingana na idara ya hali ya hewa ya Ujerumani, mvua kubwa na mafuriko iliyoshuhudiwa katika majimbo mawili imetatiza shughuli za kawaida kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita na mvua nyingi zaidi inatarajiwa kunyesha.
Jumla ya waokoaji wa dharura 40,000 wameshiriki juhudi hizo za uokoaji tangu Ijumaa. jeshi la Ujerumani pia limelazimika kuingilia kati juhudi hizo wakati ambapo mito katika jimbo hilo la Bavaria ikiwa inazidi kufurika.