Mabishano fedha za Maliasili na Utalii kumalizwa na Kamati ya Bajeti

Dodoma. Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema suala la mgawanyo wa fedha za nyongeza ya Sh19 bilioni, wizara imepanga Sh14 bilioni ziwe za matumizi ya kawaida, sasa litapelekwa kwenye Kamati ya Bunge ya Bajeti.

Spika amesema hayo baada ya kupokea marekebisho ya pande mbili, Serikali na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Amesema wizara imezungumzia marekebisho ya Sh19 bilioni na siyo Sh14 bilioni ambazo zimeelekezwa kwenye matumizi ya kawaida (OC), huku kamati akizungumzia marekebisho ya Sh14 bilioni.

Waziriwa Maliasili na Utalii amesema wizara imefanya marekebisho matumizi ya Sh14 bilioni aliyoelekezwa kwenye matumizi mengineyo (OC) huku kwenye maendeleo zikielekezwa Sh5 bilioni.

Kairuku amesema hayo jana wakati akifanya majumuisho ya hoja mbalimbali za wabunge zikiwamo za fidia za uharibifu na vifo zinazosababishwa na wanyama wakali.

Pia, kuhusu askari wa hifadhi wanaotuhumiwa kuwapiga risasi wananchi hadi kusababisha vifo, kuondoa viingilio kwa wafanyakazi wa ndani ya hifadhi na kupunguza ada kwa waongoza watalii mlimani.

Akijibu hoja ya fedha za nyongeza Sh19 bilioni ambapo  wizara iliamua mgawanyo wa Sh14 bilioni ziende kwenye matumizi mengineyo na Sh5 bilioni ziende kwenye miradi maendeleo.

Kamati ilipinga mgawanyo huo na kutaka fedha hizo zielekezwe kwenye utafiti huku wabunge Ester Bulaya (Viti Maalumu) na mbunge wa Makete, Festo Sanga nao wakipinga mgawanyo huo.

Pia, Kairuki amesema wizara imekubaliana na hoja za wabunge kuhusu utoaji wa kifuta jasho na kifuta machozi kwa wanaoathirika na wanyamapori.

“Waheshimiwa wabunge tumepokea mapendekezo yenu ikiwamo fidia kwa walioharibiwa mazao, watalipwa hata wa chini ya heka moja watalipwa,” amesema.

Pia, amesema ada kwa wanaopandisha watalii Mlima Kilimanjaro ambayo ni Dola 2,000 za Marekani sasa watatozwa Dola 1,000.

Kuhusu wafanyakazi kwenye makambi au hoteli zilizomo ndani ya hifadhi kutozwa kiingilio kwenye geti, amesema wafanyakazi hao hawatatozwa kiingilio na kwa magari ambayo yanatozwa ada ya mwaka kuingia hifadhini, watakaa na kulifanyia kazi.

Kairuki pia amesema hoja ya leseni kwa waongoza watalii sasa itakuwa Sh100,000 kwa miaka mitatu na itatozwa kwa fedha za Tanzania.

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, ilisomwa na mwenyekiti wake Timotheo Mnzava, ndiyo iliyoibua utata huo.

Fedha za matumizi ya mengineyo (OC) za Sh14 bilioni kati ya Sh19 bilioni zilizoongezwa kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii, zimekataliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, huku wabunge wakisema fedha hizo zihamishiwe kwenye maendeleo.

Related Posts