Mkenya alie rekodiwa akimpiga polisi ashtakiwa

Dereva Mkenya mwenye umri wa miaka 19 ambaye polisi wanasema alirekodiwa akimpiga polisi wa trafiki kwenye barabara katika mji mkuu, Nairobi, amefunguliwa mashtaka ya wizi kwa kutumia vurugu.

Video ya tukio hilo, ambayo imesambazwa sana, ilionyesha mshambuliaji akimshambulia polisi kwa mateke na makofi wakati wa tukio la Jumapili.

Kisha alitoroka kutoka eneo la tukio baada ya wananchi kuingilia kati na kumuokoa polisi huyo.

Ian Njoroge, mwanafunzi wa chuo kikuu, Jumanne alikanusha mashtaka yote ambayo pia ni pamoja na kusababisha madhara makubwa na kukataa kukamatwa, ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma ilisema.

Upande wa mashtaka ulisema mshukiwa alimpora polisi simu ya rununu na betri ya kifaa cha mawasiliano cha polisi, kulingana na chapisho kwenye X, zamani Twitter.

Sheria ya Kenya inatoa hukumu ya kifo ya lazima kwa watu wanaopatikana na hatia ya wizi wa kutumia nguvu.

Mshukiwa huyo pia anadaiwa kusababisha kizuizi cha madereva wengine wa magari wakati wakiendesha na kubeba abiria kupita kiasi.

Mawakili wa utetezi walisema mteja wao alidhulumiwa nyumbani kwake wakati wa kukamatwa, tovuti ya habari ya Citizen inaripoti.

Mahakama ilikubali upande wa mashtaka siku moja kumzuilia mshukiwa inapotayarisha kesi yake.

Related Posts