Aweso, Bashe wakutana kuweka mikakati maelekezo ya rais Samia

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso(MB) amefika ofisi ya Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe(MB) Wizara ya Kilimo jijini Dodoma kwa lengo la kikao kazi cha pamoja kuweka mikakati juu ya ushirikiano katika utekelezaji wa Miradi ya Maji iendane na kutoa suluhu eneo la kilimo cha hususani cha Umwagiliaji.

Kikao hiki ni sehemu ya Maelekezo ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliotoa kwa Wizara hizi kufanya kazi na kutekeleza miradi sambamba ili iwe na tija kwa matumizi ya binadamu pamoja na kilimo cha umwagiliaji.

Aidha akizungumza Mhe Aweso amesema tayari Wizara ya Maji imeakwishaanza mkakati mahususi katika utekelezaji wa miradi wake kuwa na mpango maalum wa kunywesha Mifugo na kazi hiyo inaendelea vema kwa kushirikiana na Wizara ya Mafugo na Uvuvi na kuweka bayana kwamba ni wakati sahihi wa kuendeleza mpango huu kwa Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji.

Naye Mhe Bashe amesema sasa ni wakati wa Menejimenti na wataalam wa Wizara ya Kilimo na Wizara ya Maji kuwa na kikao cha Pamoja ili kuwa na mpango mkakati wa utekelezaji wa Maono haya ya Mhe Rais.

Related Posts