Taifa Gas Yapewa Tuzo Kutambua Jitihada Zake Utunzaji wa Mazingira Nchini
Dodoma: Juni 5, 2024:
Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amekabidhi tuzo maalum kwa kampuni ya nishati
ya gesi ya kupikia ya Taifa Gas Limited ikiwa ni ishara ya serikali kutambua juhudi
za kampuni hiyo katika utunzaji wa mazingira sambamba na kuunga mkono kampeni
ya kumtua mama kuni kichwani inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu
Hassan. Kampeni hiyo inalenga kuwasaidia na kuwawezesha wananchi kuifikia nishati hiyo kwa urahisi.
Dk Mpango amekabidhi
tuzo hiyo kwa Meneja Mkuu wa Taifa Gas Devis Deogratius leo jijjini Dodoma
kwenye kilele cha Maadhimisho wiki ya Mazingira iliyofanyika jijini humo na kuhudhuriwa na viongozi
wengine wa kitaifa akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Dkt.Seleman Jafo, Naibu Spika wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu pamoja na wadau
wengine wa mazingira.
Akizungumzia tuzo hiyo
kwa niaba ya Kampuni ya Taifa Gas, Deogratius aliishukuru serikali
kwa kutambua jitihada za kampuni hiyo katika uwajibikaji wake kwa jamii ikiwemo
kuiunga mkono serikali na viongozi wake waandamizi katika kufanikisha adhma ya kuandaa
taifa linalotegemea nishati safi ya kupikia kwa kuendelea kutoa mitungi ya gesi
na elimu ya matumizi ya gesi lengo likiwa ni kupunguza matumizi ya kuni na mkaa
miongoni mwa wananchi mijini na vijijini.
“Kuanzia
mwaka jana hadi
sasa, Taifa Gas tumegawa bure mitungi 20,000 yenye thamani ya Tsh .1.52
bilioni
kwa watanzania wenye mahitaji kwa ajili
ya kuendeleza kampeni hii ya nishati safi nchini. Serikali ina malengo
ya kuhakikisha
tunafikia nchi yenye nishati safi ifikapo 2034, hivyo kampuni ya Taifa
Gas tutaendelea kuunga mkono juhudi hizi ili tuweze kufikia
malengo ya pamoja” Alisema Deogratius.
Alisema kampuni hiyo
mbali na kutoa mitungi ya gesi bure kwa
Watanzania, inaendelea na mpango wake wa kutoa elimu kuhusu nishati safi sambamba
na kutoa fursa za kiuchumi kwa watanzania ambao wangependa kuwa mawakala wa
kampuni hiyo kote nchini.
Katika muendelezo wa
kampeini ya utunzaji wa mazingira, Deogratius alisema kampuni hiyo imejipanga
kuhakikisha kwamba kila Mtanzania mwenye
nia ya kutumia nishati safi ya gesi anapata fursa hiyo kupitia vituo vya
usambazaji ya taifa gas ambayo vinapatikana kila mkoa kote nchini.
“Tanzania inapoteza
takriban ekari 400,000 za misitu kila
mwaka kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa na Taifa Gas ni
miongoni mwa kampuni ambazo zimejitolea kusaidia serikali katika jitihada hizi.’’
alisisitiza
Makamu wa Rais Dk
Philip Mpango (wa pili kulia) akikabidhi
tuzo maalum kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya kuzalisha na kusambaza nishati ya gesi
ya nyumbani ya Taifa Gas Limited, Devis Deogratius (Kushoto) ikiwa ni ishara ya
serikali kutambua juhudi za kampuni hiyo katika utunzaji wa mazingira sambamba
na kuunga mkono kampeni ya kumtua mama kuni kichwani inayoongozwa na Mheshimiwa
Rais Samia Suluhu Hassan. Tuzo hiyo imekabidhiwa leo jijjini Dodoma kwenye
kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira yaliyofanyika jijini humo. Wanaoshuhudia ni pamoja
na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa tatu Kulia),
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi
Muungano na Mazingira Dkt.Seleman Jafo (Kulia)na Naibu Spika wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (wa nne kulia)