TETESI ZA USAJILI BONGO: Azam yatua Yanga, Kipa azam …

KIPA wa Yanga, Aboutwalib Mshery amemaliza mkataba wake ndani ya kikosi hicho huku akisubiria viongozi kujua hatima yake msimu ujao, huku klabu ya Azam ikitajwa kumfukuzia.

Duru za kimichezo zinasema wawakilishi wa mchezaji huyo, tayari wameanza mazungumzo na klabu kadhaa huku ikielezwa Azam ni kati ya zinazomhitaji kwa kilichoelezwa mipango ya kumrejesha Aishi Manula huenda ikakwamwa.

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Geita Gold, George Mpole ameanza kufuatiliwa na timu mbalimbali nchini kwa ajili ya msimu ujao.

Mfungaji bora huyo wa Ligi Kuu msimu wa 2021-2022 alikuwa akicheza FC Lupopo ya DR Congo ambako amemaliza mkataba na sasa klabu za Pamba, KenGold na Simba zinatajwa kuzungumza naye ili kumnasa.

BEKI wa timu ya taifa, Taifa Stars, Miano van den Bos anayeichezea Villena ya Hispania amepata nafasi ya kufanyiwa majaribio katika Klabu ya Elche CF inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini humo (La Liga2).

Elche imekuwa ikivutiwa na kiwango cha kinda huyo aliyezaliwa na kukulia Uholanzi tangu mwanzoni mwa msimu.

BAADA ya kuwa na msimu mzuri akiwa kwa mkopo Azam FC akitokea El Merrikh, kipa Mohamed Mustafa anayetakiwa kurudi Sudan kwa waajiri wake, ni kama amenogewa na maisha ya Chamazi sasa anaripotiwa kuwasikilizia mabosi wa timu hiyo kuona kama wanaweza kumsajili jumla katika dirisha hili la usajili.

Related Posts