TETESI: Manu Lobota atajwa Yanga

YANGA inahusishwa kuhitaji huduma ya straika mkongomani, Emmanuel Bola Lobota kutoka Ihefu.

Lobota aliyejiunga na Ihefu katika dirisha dogo la msimu uliopita akitokea FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo amekuwa kwenye mawindo ya Yanga tangu mwanzoni mwa msimu uliopita.

Nyota huyo kabla ya kutua Ihefu, alishafanya mazungumzo na Yanga na Singida Fountain Gate, lakini baada ya mgawanyiko wa Singida FG ndipo akaibukia Ihefu ambayo inaelezwa imeshikilia dili la kujiunga na Yanga ili walete jembe jingine jipya.

Mwanaspoti limedokezwa kuwa tayari mshambuliaji huyo yupo hatua nzuri katika mazungumzo na Yanga na kama mambo yataenda sawa, basi msimu ujao atavaa jezi za Wananchi ambao wanashikilia mataji ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho kwa msimu wa tatu mfululizo.

Related Posts