LYRA IN AFRICA imekuja na mpango wa kuinua vijana wenye ubunifu na teknolojia

Uhaba wa walimu wenye ujuzi wa kufundisha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), umetajwa kuwa kikwazo cha wanafunzi wa shule za sekondari mkoani Iringa kujifunza teknolojia hiyo.

Karibu shule nyingi za sekondari za Mkoa wa Iringa zimeanzisha madarasa ya Tehama kutokana na uwepo wa kompyuta.

shirika linalolenga kukuza ujuzi wa Tehama shuleni la Lyra Tanzania liligawa kompyuta 320 kwa shule kumi za sekondari 10 za Mkoa wa Iringa na kufanikiwa kuanzisha Jukwaa la Tehama Mkoa wa Iringa.

Akizungumza katika maonyesho ya bunifu mbalimbali za kidijitali, Meneja wa Mradi wa Mifumo ya Kujifunza Kidijitali kutoka Shirika la Lyra, Nora Mkenda amesema uhaba wa walimu ndio kikwazo

“Changamoto kubwa ni uhaba wa walimu wa Tehama, hili ni tatizo kubwa na linaathiri wanafunzi wenye vipaji vya ubunifu kushindwa kuendeleza bunifu zao,” amesema.

Wamesema mfumo huo unatoa huduma ya maji kidijitali ambapo mteja atalazimika kuweka sarafu ya Sh200 na kupata huduma moja kwa moja bila kuwepo kwa mtoa huduma yeyote.

Related Posts