RAFIKI WA MWALIMU NI MWALIMU MWENZAKE – DKT. MSONDE

Naibu katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu) Dkt Charles Msonde amewataka walimu wa shule za msingi na sekondari kuwa na tabia ya kupendana wao kwa wao na kuwa marafiki kwa kushirikiana katika maeneo mbalimbali ili kuweza kudfanikisha mambo yao kwa Pamoja.

Dkt. Msonde amesema haya katika kikao cha Pamoja kati ya walimu hayo, Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule na wawakilishi kutoka Chama Cha Walimu Tanzania kilichofanyika katika Shule ya sekondari ya Magreth Sitta katika Halmashauri ya Urambo Mkoani Tabora.

“Tufute kauli ya kumdhalilisha mwalimu, kuna kauli moja inasema adui wa mwalimu ni mwalimu tunataka tuifute kauli hiyo, badala yake tuseme kwamba rafiki wa mwalimu ni mwalimu hivyo watupasa kupendana, kushirikiana na kusaidiana sisi kwa sisi katika mambo mbalimbali kwani sote tumesomea walimu”

Dkt Msonde amewataka pia Maafisa Elimu Msingi na Maafisa Sekondari kuonyesha upendo na umoja huo kwa walimu wa kawaida ili kuweza kufanikisha mahitaji mbalimbali ya walimu bila ubaguzi.

Aidha Dkt Msonde amewataka walimu kuwa wabunifu kwa kutafuta mbinu mbalimbali za ufundishaji na ujifunzaji ili waweze kuwasaidia wanafunzi wanaofanya vibaya darasani na kuachana na dhana hasi na kuwa na mtazamo chaya kuwa wanaweza kufanya vizuri endepo mwalimu wakiamua kuwafundisha.

Kwa upande wake Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Urambo mhe. Magreth Sitta ameishukuru ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuendelea kuboresha na kusimamia miradi mbalimbali ya elimu katika Halmashauri ya Urambo na kuwaomba walimu kuendelea kutimiza majukumu yao ili kuwasaidia wanafunzi kutimiza malengo yao nay a serikali kwa ujumla.

Akitoa neno la shukrani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Urambo Bi. Grace s. Quintine amesema kama halmashauri itaendelea kusimamia Maslahi ya walimu wote katika halmashauri ya Urambo ili waweze kufurahia kutekeleza majukumu yao ya kila siku la kulijenga Taifa.

Related Posts