Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Kaimu Mkurugenzi wa Chuo Cha Ufundi Veta Kanda ya Kati Bwana Mataka Ramadhani Mataka akieleza mafanikio ya Miaka mitatu ya Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Raisi huyo anatoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1.6 kila mwaka kwa Veta Mkoa wa Dodoma ili Vijana wa Kitanzania waweze kupata mafunzo ya ufundi stadi ili wakitika pale waweze kujiajiri au kuajiriwa.
Mataka ameyasema hayo mapema Leo hii Juni 11,2024 Jijini Dodoma katika mkutano wake na Wanahabari wakati akielezea mafanikio ya miaka mitatu ya Uongozi wa Dkt Samia kwa Veta upande wa mkoa wa Dodoma ambao huratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Na kuongeza kuwa Vijana wanaopata mafunzo ya ufundi stadi Veta ni 1878 kwa wale wa bweni na kutwa na wanatakiwa kulipa laki 9 kwa gharama na mambo mengine lakini mzazi analipa laki moja na elfu ishirini tu na ambayo hiyo ni sawa na elimu bure mzigo unaobaki wote unabebwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya miaka yote mitatu.
“Sasa katika vijana 1878 hao ni vijana wa bweni kwa mkoa wa Dodoma sasa ukizidisha vijana hao wanaokaa bweni na kutwa hiyo kali 9 uzidishe kwa idadi hii utapata kila mwaka kwa mkoa wa Dodoma Raisi anatoa zaidi ya 1.6 bilioni kwa Veta ili vijana wa kitanzania kuweza kupata mafunzo ya ufhndi stadi, hiki ni eneo linalomuwezesha kijana kupata ufundi akitoka pale aweze kujiajiri au kuajiriwa,haya ni mafanikio makubwa kwa Veta mkoa wa Dodoma ndani ya uongozi wa Dkt Samia”.
“Sote tunatambua kuwa ada ya Veta kwa mwaka ni elfu 60 ,ada ya bweni na kijana kufanya vitu vyote ikiwemo chakula ni elfu 60 pia hivyo kwa mwaka mzima kija a analipa laki moja na elfu 20, lakini gharama ya kumfundisha anayelala bweni,chakula na vitu vyote ni zaidi ya laki 9. Sasa mzazi analipa laki moja na elfu ishirini tu ambapo ni sawa na elimu bure japo Mh Raisi hajasema hivyo,lakini ukichukua laki 9 ukatoa laki moja na elfu 20 mzigo wote unaobaki unabebwa na Mhe Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka hiyo mitatu”.
Sambamba na hayo pia ameongeza mafanikio katika eneo la kutahini wanafunzi wa ufundi katika miaka mitatu ya Dkt Samia ambapo amesema Veta kabla ya miaka hii wanachuoa walikuwa hawafiki 3800,lakini kwasasa wanao 5373 kwa miaka mitatu hii,hivyo wameongeza idadi ya elfu 3373 kutoka 3800 ambayo hii pia imechangiwa na Serikali kutoa kwa Veta ili vijana waweze kupata mafunzo haya ya ufundi Stadi.
“Mafanikio pia yapo katika suala la kutahini wanachuo kabla ya miaka hii wanachuo walikuwa hawafiki 3800 lakini hapa ninapoongea ni elfu 5373 sasa hii ni kwa miaka mitatu,kilichofanyika tumeongeza idadi ya wanafunzi elfu 3373 kutoka 3800”.
Aidha Bwana Mataka ameongelea suala la matarajio yao kama Veta kwa mkoa wa Dodoma ambapo amesema kuugeuza Mkoa kuwa Kinara kwa kutoa Vijana wenye sifa nzuri na wenye ushindani katika soko la ajira na kuhakikisha baadhi ya Viwanda na baadhi ya Sekta zinafanya kazi kwa ubora zaidi kuongeza uchumi kwa kuitumia Veta.
“Matarajio yetu ni kugeuza mkoa wa Dodoma kuwa Kinara kuwa ni Hub ya kutoa vijana wenye sifa nzuri,vijana ambao wataenda kutumika kwenye viwanda vingine tifauti na mkoa wa Dodoma, poa tunatarajia kupandisha Kozi fupi nyingi, Uwezo wetu ni kufikisha zaidi ya vijana elfu 10,000 lakini namba si hoja kwetu, hoja ni kijana a akubariki vipi katika soko la ajira”.
“Tuna matarajio makubwa sana kwa mkoa wa Dodoma kwa miaka hii 4 ikiwa ni pamoja na kuhakikisha baashi ya viwanda na baadhi ta Sekta inafanya kwa ubora zaidi kuongeza uchumi kwa kuitumia Veta,lakini hata wakulima Veta imeingilia katia kuhakikisha uchakataji mzima wa mvinyo u akuwa vizuri,mitaala iweje na tunashea na wenye viwanda wenyewe nadhani hii itafanya mkoa wa Dodoma kunawili kwa vijana na hata ambao sio vijana kwani veta unachukua hata wale wenye umri mkubwa ili mradi uje kupata ujuzi na kufanya maisha yaendelee na kipato kiongezeke”.
Zipo faida za kupata mafunzo ya Ufundi Stadi ikiwa ni pamoja na Kujiajiri,Kuajiriwa na Kuajiri.