TETESI ZA USAJILI BONGO: Simba yamfuata ndugu yake Aziz Ki

IMERIPOTIWA kwamba, Klabu ya Simba ipo kwenye mazungumzo na beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Burkina Faso na FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo, Valentin Nouma kwa ajili ya kuipata huduma yake.

Simba ambayo imepanga kujiimarisha zaidi kuelekea msimu ujao, inaamini kwamba beki huyo anayecheza kikosi cha Burkina Faso sambamba na kiungo wa Yanga Stephane Aziz Ki, anaweza kuwa mtu sahihi kwao.

Uamuzi wa Simba kusaka beki wa kushoto umekuja baada ya kumtumia kwa muda mrefu nahodha wao, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye anaonekana mpinzani wake ameshindwa kupatikana.

 Mbali na Nouma, Simba hapo awali ilikuwa ikitajwa kuwa kwenye mazungumzo na beki Joyce Lomalisa aliyemaliza mkataba ndani ya Yanga ambapo timu hiyo inaangalia uwezekano wa kumpata beki wa kushoto kwenda kusaidiana na Tshabalala.

Related Posts