SHIRIKA lisilo la kiserikali La Forum CIV Kushirikiana Taasisi ya Kukuza Sanaa Nafasi Art Space zimefanikiwa kuwezesha wasanii kupewa mafunzo kwa kutumia sanaa zao kuwa wana harakati ili waende kuisemea jamii inayo wazunguka kutokana na changamoto mbalimbali zinazo wakumba.
Akizungumza na Wanahabari Mkurugenzi wa Nafasi arts space Lilian Hipolyte amesema ushirika huo unalenga kuwawezesha wasanii katika taaluma mbalimbali za ubunifu kuwapa zana na ujuzi wa kutumia nguvu ya sanaa na kwaajili ya mabadiliko ya kijamii.
“Shirika hilo la limeona kuna haja wasanii hao kuacha kuimba zisizo na maadili na badala yake kutumia sanaa zao ili kuiwezesha jamii kupaza sauti zao kwa viongozi wao juu ya changamoto zinazowakabili.”
Nae Meneja program kutoka Taasisi ya Forumciv Jackson Obare amesema inajivunia kuzindua uzinduzi wa Ushirika wa Sanaa nchini Tanzania, kuashiria mpango wa mwanzo ndani ya mandhari ya kisanii nchini.
Aidha Obare amesema kuwa Mafunzo hayo yameanza ramsi Juni 10 hadi Septemba 30, 2024, ushirika huu wa mabadiliko unalenga kuwawezesha wasanii 10 tofauti katika taaluma mbalimbali za ubunifu, kuwapa zana na ujuzi wa kutumia nguvu ya sanaa kwa ajili ya mabadiliko ya kijamii, dhana iliyojumuishwa na neno ‘ usanii.’
Hata hivyo obare ameongeza kuwa Ushirika wa Sanaa unawakilisha fursa muhimu kwa wasanii kujihusisha kwa kina na maswala muhimu ya kijamii, kutumia talanta zao za ubunifu ili kuleta matokeo yenye maana na kuhamasisha mabadiliko chanya.
Pia ameeleza kuwa Katika kipindi cha miezi mitatu, washiriki watapitia mafunzo ya kina, ushauri, na miradi shirikishi, na hivyo kuhitimishwa na onyesho thabiti la kazi na maono yao kwa jamii yenye usawa na haki.
Kwa Upande wa Mnufaika wa mafunzo hayo Ayoub Kondwe ameeleza namna walivyovutiwa na kozi hiyo ambapo wameeleza namna watakavyoenda kuisemea jamii kwa kupitia vipaji vyao.
Mkurugenzi wa Taasisi ya ‘Nafasi arts space’ Lilian Hipolyte akizungumza na Wanahabari wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Harakati kwa Wasanii (ARTIVISIM ) inayolenga kuwajengea uwezo wasanii kuongeza kipato
Mkongwe wa Muziki nchini John Kitime akitumbuiza katika Uzinduzi wa Mafunzo(ARTIVISIM) ya kuwawezesha wasanii kuongeza vipato vyao
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nafasi arts space Lilian Hipolyte akiwa sanjari na Meneja mradi kutoka (FORUMCIV) Jackson Obare wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Mafunzo ya miezi mitatu kwa Wasanii wenye Lengo la Kuwaongezea Vipato vyao kupitia sekta ya sanaa zao