Gairo yafikia asilimia 65 upatikanaji wa maji

Serikali kupitia RUWASA Wilaya ya Gairo imefanikiwa kufikisha huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 65 Kwa wakazi wa wilaya hiyo huku mpango kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2025.

Meneja wa RUWASA wilaya ya Gairo Mhandisi Gilbert Isaack amesema Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya maji ambapo tayari mabomba yenye Thamani ya milioni 700 yamesambaza tayari kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha Mhandisi Gilbert Isaack amesema kuwa mabomba hayo yenye thamani ya shilingi milioni 700 yaliyotolewa wilayani humo kutoka serikalini kuu yanakwenda kuboresha hali ya upatikanaji maji safi na salama wilayani humo na kufikia asilimia 75.

Mhandisi Gilbert amesisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wa mijini na vijijini waoishi wilayani humo wanapata huduma ya maji yenye uhakika

Anasema Serikali inatambua changamoto ya maji katika eneo hilo ambapo hadi mwishoni mwa mwaka huu 2024 watafikia asilimia 75 na kufika mwaka 2025 watafikisha kwa asilimia 95.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wanaoishi wilayani Gairo wamesema kuwa wanaishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuboresha huduma ya maji kwani hapo awali walikuwa wanapata changamoto ya kutumia maji ambayo pia hutumiwa na mifugo hali ambayo imepelekea kuhatarisha afya zao

Jane Amin mmoja wa wakazi Gairo anasema wanalazimika kuamkia usiku saa Tisa ili kuwahi foleni ya maji na wakati mwingine wanapata maji mara mbili Kwa wiki hivyo uboresha wa huduma hiyo italeta manufaa kwao.

Related Posts