Ujenzi wa vyuo vya ufundi kuanza Ushetu

Serikali imesema kuwa kuanzia mwaka wa fedha 2024/2025 imeadhimia kujenga vyuo vya fundi katika majimbo na maeneo yote ambayo hakuna Vyuo vya ufundi na Veta.

Akiongea bungeni jijini Dodoma Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh.Omary Kipinga wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani alilouliza “ni lini Serikali itaanza ujenzi wa shule ya ufundi katika halmashauri ya Ushetu?”

“Adhima ya serikali ni kuhakikisha kuwa majimbo yote ambayo hakuna vyuo vya ufundi vinajengwa kupitia mwaka wa fedha 2024/2025, kwahiyo niwatoe wasiwasi wananchi wa Ushetu na Mhe Cherehani kuwa Serikali ipo kazini na ujenzi wa shule utaanza mwezi wa saba katika mwaka mpya wa fedha” Naibu Waziri Omary Kipinga

Related Posts