TETESI ZA USAJILI BONGO: Mzamiru ana jambo lake Simba

KLABU ya Simba iko kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili kiungo nyota wa kikosi hicho, Mzamiru Yassin.

Mkataba wa kiungo huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar aliyemaliza msimu akiwa na asisti nne umefikia ukingoni na tayari wawakilishi wa Mzamiru wameanza mazungumzo ili asaini dili jipya na miamba hiyo.

Klabu mbalimbali za Azam FC na Singida Black Stars (Ihefu FC) ni miongoni mwa zilizokuwa zinahitaji saini za kiungo huyo anayeichezea timu hiyo kwa misimu nane mfululizo ili kuboresha vikosi vyao.

Nyota huyo alisajiliwa Simba msimu wa mwaka 2016 sambamba na Shiza Kichuya na tangu hapo amekuwa mmoja ya viungo wa kizawa anaochuana na mastaa wa nyota wa kigeni katika nafasi hiyo na msimu huu alikuwa lulu mbele ya makocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’, Abdelhak Benchikha na Juma Mgunda.

Related Posts