KITUO CHA POLISI MKIWA KUKAMILIKA

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini itaunga mkono jitihada za wananchi,wadau na Mbunge kupitia mfuko wa Jimbo katika ujenzi wa Kituo kidogo cha Polisi kilichopo Kata ya Mkiwa ili kituo hicho kikamilike na kisaidie kuimarisha usalama wa wananchi.

Mtaturu ameuliza swali hilo Juni 12,2024,Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu.

“Kata ya Mkiwa tumeanza ujenzi wa kituo kidogo cha polisi ambacho ni kituo cha mkakati ,mimi kama Mbunge kupitia Mfuko wa Jimbo nimechangia Milioni 5,wananchi na wadau wameshirikiana pia,Je ni lini serikali itatuunga mkono ili kumalizia kituo hiki kwa ajili ya usalama wa wananchi wetu,?”.amehoji.

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Daniel Sillo amesema katika Mwaka wa Fedha wa 2024/2025, serikali imetenga Sh.Bilioni 3.8 kwa ajili ya kumalizia maboma yote 77 yaliyojengwa na wananchi.

“Naomba nimuhakikishie Mh Mbunge baadae tuonane ili tuone pengine kituo chake kipo katika maboma haya hivyo tuweze kumalizia katika mwaka wa fedha wa 2024/2025,”.amesema.

Related Posts