Wasanii wanamchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa rai kwa wasanii kupitia kazi zao za sanaa kuweka jumbe za matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ili wananchi waliowengi wapate kuelewa matumizi ya matokeo ya sensa baada ya mafanikio makubwa ya takwimu za sensa yaliyopatikana baada ya kukamilisha zoezi la kuhesabu watu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Chalamila ametoa kauli hiyo leo Jumatano wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa wasanii wa Mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Kiramuu, Mbezi-Beach.

Chalamila akifungua mafunzo hayo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyowekeza na kujali wasanii hapa nchini kwa kuanzisha mfuko maalum wa wasanii

Sanjari na hilo RC Chalamila amesema wasanii ni kundi muhimu hivyo ni vizurii kabla hawajadhibiti kazi ya msanii, kufanyike mjadala kujua historia yake na mambo mengine na hatimaye ajengewe uwezo zaidi.

“Wasanii wanaweza kuwasilisha kwa watu wengi ujumbe mgumu kwa wepesi na watu wakauelewa” Amesema RC Chalamila.

Amesema mafunzo hayo kwa wasanii yameratibiwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu ambapo kundi la wasanii kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambao ni kundi la kwanza kupatiwa mafunzo hayo.

Amesema kutokana na nguvu kubwa ya wasanii katika jamii ni ukweli pasina shaka ujumbe wa matumizi ya matokeo ya Sensa unakwenda kuifikia idadi kubwa ya watu nchi nzima.

Related Posts